To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Monday 31 January 2011

The 5 toughest tests of a relationship!!

copyright;maisha blog

1. Planning a wedding
Being engaged is hugely exciting but once the dust settles many couples find the realities of joint event-planning less than scintillating. It’s a bit like working together – and that’s a whole different ball game from a romantic relationship. You need to treat this like you would a new work colleague: be patient, understand each other’s strong points, don’t expect the earth, and make your expectations and limitations clear from the start.

The dynamic differs from couple to couple, but there are usually issues: one of you might expect the other to do everything, or could be a control freak who takes over. Indecisive control freaks are particularly hard to handle: we suggest arranging regular meetings with bullet pointed agendas. Yes, it sounds boring but if you treat a wedding as a work project, you’ll get things done more quickly and have more time left to get excited about the fun stuff. This is your shared vision: be creative, share your dreams, make them happen – and make time to relax when the W word is definitely off the agenda.

2. Losing a job
.
Unfortunately, more and more of us will know how losing a job feels, but it needn’t be a disaster. Some of the greatest minds in history have been rejected countless times before they found their niche, and you can too.

If one or even both of you find yourselves between jobs, use the opportunity to make a list of your hopes and dreams. Think about your long-term goals, which are much easier to visualise when you’re not stuck in the daily grind with office politics weighing you down. This might be a chance to move house, city or even country together; you may find a joint project you can embark on.

But remember: this is also a time that can make a partner feel very vulnerable and lacking in confidence. Someone who’s lost a job needs sympathy and a good listener before they need a motivating pep-talk. Whatever you do, make sure you find quality time to make each other feel loved, supported and – when the time is right – capable and full of career promise

3. Losing a relative
Bereavement affects everyone differently: there’s no right or wrong way to grieve. But it’s likely that if you or your partner loses someone close, then your intense and ever-changing emotions will affect your relationship. We tend to take out our stresses on those closest to us, so the most important thing is to be open and honest about your feelings before you get to the “snapping” point. Try to share your thoughts while you’re sober and calm and remember that this is another time to give each other lots of physical love and affection – there may be a void that needs filling.

However devastating a loss is, it can throw a spotlight onto your relationship and show just how supportive and understanding your partner can be. If he really comes through for you now, you know he’s a keeper and the shared experience will bring you closer and bind you together forever.

4. Having an affair
Here’s a tricky one. Many would say that a dalliance signals the end of a partnership, that it’s a fatal sign that something – or someone - is essentially wrong. That’s often the case, but not always. Many wonderfully happy couples have patched it up after an affair and you have to take it on a case-by-case basis. Different couples have different rules, and a semi-conscious drunken one-night stand isn’t the same as a long-term love affair. Sadly, many people turn to others out of frustration with aspects of their relationships – aspects they haven’t felt able to confront their partner about.

However hard it may seem, the key is communication. Remember that talking through your worries could prevent a relationship meltdown – although we do suggest you pick your time and place (no-one likes a bleater). If you’re at the beginning of a relationship, vow to tell each other if anything happens with another party – and stick to that. Honesty brings you closer and if you decide to part ways, so be it. But don’t let a lack of communication bring a potentially strong relationship down.

5. Buying a house


This is said to be one of the most stressful situations anyone can suffer, and with reason. Horrid paperwork, agonising decisions, hard graft, social sacrifices and the futile desire for a crystal ball… Sharing a process like that with anyone is tricky and with a partner it can be even harder as so many emotions are involved.
Don’t shoulder the burdens yourselves: talk to other friends who’ve been through the same. And accept that buying property is going to haemorrhage more cash than you’ve ever spent on designer handbags. Make sensible, informed decisions – now is not the time to be rash. But try to keep a perspective on the big picture: you are in this for the long haul, and that takes sacrifices. Sacrifice ain’t fun in the short term, but it’s what could make you madly happy in five or 10 years time. You’ve got to be in it to win it. Good luck!

Source;handbag.com

Maggid na neno la leo!!

copyright;maisha blog
Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi Mdomoni!


Ndugu Zangu,

HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake.
Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe.

Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka,kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele.

Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi.
Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ’ HATULIPI!, HATULIPI! ’- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu. Na Hilo Ni Neno La Leo.




Maggid
Iringa,
Jumatatu, Januari 31, 2011
mjengwa

Monday 24 January 2011

Bomb blast killed at least 10 people and injured 20 in Russia today!!

A spokeswoman for the investigative committee of the federal prosecutor's office put the number of casualties at about 20, citing preliminary information, and said the cause of the blast was unknown.
Moscow suffered its worst attack in six years in March 2010 when two female suicide bombers from Russia's volatile Dagestan region set off explosives in the metro, killing 40 people.
Source;news of the World

Monday 17 January 2011

MOTIVATION OF TODAY!!

copyright;maisha blog
All a Man needs is a patient woman to stick by and watch his dreams fall into place and to quit nagging. Do you think she knew he would become the US president at this time? I don’t think so, but she stuck with him and his VW beetle anyway.



Concentrate on this sentence; "To get something you never had, you have to do something you never did." When God takes something from your grasp, He's not punishing you, but merely opening your hands to receive something else. Concentrate on this sentence. "The will of God will never take you where the Grace of God will not protect you." Something good will happen to you today, something that you have been waiting for, or to hear. Please do not break. Just 27 words, God our Father, walk through my house and take away all my worries and illnesses and please watch over and heal my family in Jesus' name, Amen. This prayer is so powerful.  A blessing is coming to you in form of a new job, a house, a relationship or financially. Do not break or ask questions. This is a test. Does God come first in your life? 

Wadau wa jijini Mbeya naomba maelezo ya taswira hiyo tafadhali!!

copyright;maisha blog

HATIMAYE MH.WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA UDOM...WAHADHILI WAAHIDI KUENDELEA NA KAZI HII LEO JUMATATU.

copyright;maisha blog
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda.
WAZIRI MKUU Mh. Mizengo Pinda ameweza kusuluhisha mgogoro uliokuwepo baina ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)na wahadhiri wa chuo hicho kuhusu maslahi yao na kwamba wamekubali kuingia madarasani kuanzia leo.


Akizungumza na wanajumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) jana mchana kwenye ukumbi wa Chimwaga, Waziri Mkuu alisema matatizo yaliyojitokeza katika chuo hicho ni mlundikano wa mambo ambayo yamekuwepo siku nyingi lakini mengi ni ya kiutendaji tu na yanaweza kuisha bila kupoteza muda mwingi.
“Nimeongea na viongozi wa UDOMASA na kuwaahidi kuwa madai yenu ya posho yanaweza kukamilika mwezi Februari, nilitaka yaishe mwezi huu lakini kwa taratibu za HAZINA sasa hivi wameshaanza kushughulikia mishahara ya Januari kwa hiyo marekebisho yenu hayawezi kuwahi…wameniahidi mwezi ujao yatakamilika”, alisema huku akishangiliwa.
Amesema amemwita Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aje kukagua taarifa za mahesabu ya chuo hicho ili kubaini tuhuma zilizojitokeza za watu kulipwa hundi mbili za mishahara,walioacha kazi kuendelea kuwemo kwenye payroll ya mishahara, na wengine kukosekana kabisa kwenye payroll.
“Taarifa nilizonazo ni kwamba CAG atakuwa hapa kesho… mpeni ushirikiano ili aifanye kazi kwa urahisi…, nia yetu ni kuangalia mfumo mzima wa fedha na utawala ukoje ili ikibidi uweze kurekebishwa,”alisema.
Kuhusu madai ya wanafunzi ya tatizo la maji, Waziri Mkuu alisema amemwagiza Naibu Katibu Mkuu (Fedha) Bw. John Haule ambaye alikuwepo katika ukumbi wa Chimwaga afuatilie uhamisho wa ndani wa fedha (reallocation) katika Wizara ya Maji ili zipatikane sh. bilioni 1.66 zinazohitajiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dodoma (DUWASA) kuchimba visima maeneo ya Ng’ong’ona na Ihumwa ikiwa ni pamoja na kutandaza mabomba hadi chuoni ili kupunguza shida ya maji haraka iwezekanavyo.
Pia alisema katika mipango ya muda mrefu, DUWASA pia wanataraji kupata dola za Marekani milioni 26 ambazo zitatumika kuchimba visima vingine na kujenga matanki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 za maji na hivyo kuondoa kabisa tatizo la maji chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimweleza Waziri Mkuu kwamba mahitaji halisi ya maji chuoni hapo ni lita milioni 3.5 kwa siku ambazo kati ya hizo, lita milioni 1.5 ni kwa matumizi ya wanafunzi peke yao na lita nyingine milioni mbili ni kwa matumizi ya ujenzi wa majengo unaoendelea chuoni hapo.
Mapema akizungumza na Kamati ya Makatibu Wakuu iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi, mara baada ya kuwasili mjini Dodoma jana asubuhi, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna matatizo ya malipo ya posho na mishahara kwa watumishi na wahadhiri wa chuo hicho.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Bw. Idd Mwerange alimwahidi Waziri Mkuu kwamba watarudi madarasani wakati wakisubiri madai yao yakamilishwe bali aliomba kuwe na uwakilishi wa UDOMASA katika timu ya watu watakaonana na CAG.
Akifunga mkutano huo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimwahidi Waziri Mkuu kwamba maagizo yake yatafuatiliwa na kwamba kesho (Jumatatu) menejimenti, idara ya Uhasibu na UDOMASA watakutana ili kuunda timu ya pamoja ambayo itakaa na kubainisha stahili za walimu wote ili orodha hiyo iwasilishwe kwa Waziri Mkuu mapema iwezekanavyo kwa ufuatiliaji.
Katika ziara yake ya jana, Mh. Waziri Mkuu alifanya vikao viwili, kimoja kikiwa cha uongozi wa Chuo Kikuu cha UDOM na kingine cha Serikali ya wanafunzi ambavyo vilidumu hadi saa 12.30 jioni na kumlazimu kuahirisha vikao viwili vilivyobaki hadi leo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Chuo hicho,mara baada ya kukutana na serikali ya wanafunzi, Waziri Mkuu alipangiwa kukutana na jumuiya ya wanataaluma wa Chuo hicho (UDOMASA) na kisha kufanya majumuisho katika ukumbi wa Chimwaga kwa kuzihusisha pande zote tatu.
Katika vikao vyote viwili, Waziri Mkuu alielezwa matatizo yanayokibabili chuo hicho makubwa yakiwa ni uhaba wa maji, uhaba wa walimu, vifaa vya masomo na mlundikano katika mabweni.
Waziri Mkuu kabla ya kufanya mikutano hiyo miwili, alifanya ziara chuoni kukagua miundombinu ya maji safi, maji taka,vyumba vya kulala katika mabweni ya Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii pamoja na mabweni ya skuli ya Tiba na Uuguzi pamoja na ujenzi wa visima vya maji.
IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA

Sunday 16 January 2011

SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 9,226 ZA WALIMU WA SEKONDARI NA VYUO.

copyright;maisha blog
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa wakati akitangaza ajira za ualimu mbele ya waandishi wa habari. 

Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao. Aidha, kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar (wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini) ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar. Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.

Kama ilivyobainishwa katika sehemu ya kwanza ya taarifa hii, jumla ya wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na Serikali katika mwaka huu wa fedha. Vilevile Serikali imekubali kuajiri walimu 702 (wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada) waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa Serikalini.

Hivyo, jumla ya walimu wote watakaoajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ni 9,226 wakiwemo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306. Kati ya walimu watakaoajiriwa jumla ya walimu 9,039 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika Halmashauri husika. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika Halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye Halmashauri alikopangwa na si vinginevyo. Orodha ya walimu hao na Halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye Mikoa na Halmashauri. Aidha, orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (www.pmoralg.go.tz).

Walimu wote wapya wanaagizwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika Halmashauri/ Vyuo vya Ualimu walikopangwa ifikapo tarehe 24/01/2011. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.

Mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye Halmashauri / Chuo alikopangwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na Serikali.

Baada ya kuripoti kwenye Halmashauri/Vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao Fomu maalum zenye Taarifa ya Kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form) na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, UTUMISHI pamoja na barua ya ajira ya mtumishi. Taarifa hizo zikiwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe UTUMISHI kabla au ifikapo tarehe 29/01/2011 ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika zoezi hili.

Waajiri (Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia utumishi mwema katika Sekta ya Elimu.

Imetolewa na:

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
copyright;maisha blog  
Wazo la leo!!!
Pasipo riziki hapaliki, na yaliyo pita sindwele hatuna budi kusahahu na kuganga yajayo.....jumapili njema ndugu.


President J.Kikwete has ordered 3 teams to tackle UDOM crisis!!

copyright;maisha blog

President Jakaya Kikwete has directed Chief Secretary Philemon Luhanjo to form three commissions to work on the University of Dodoma lecturers’ claims.
President Kikwete’s move, announced yesterday, comes a few days after UDOM lecturers asserted that they will not resume teaching until they meet president Kikwete to brief him about their problems.
The lecturers who are on a go-slow are claiming among other things to be paid new salaries which were approved in November last year.
The University of Dodoma Academic Staff Association chairman Paul Loisulie and the Vice chancellor of UDOM, Prof Idris Kikula said, they were aware of the president’s move.
The first commission involving the office of the Controller and Auditor General is tasked with auditing salaries of the lecturers.
The commission was expected to start its work immediately at the Treasury, auditing ‘Pay roll’ of UDOM staff.
The second commission to include permanent secretaries will probe various problems facing the university to establish the source.
The third commission will involve Tanzania Commission of Universities which will look into various academic problems facing UDOM.
The three commissions according to the UDOMASA chairperson are supposed to work on the President’s directives immediately for a speedy end to the problems still persisting at the university.
In another development Prime Minister, Mizengo Pinda is expected to meet with UDOM students today and have talks to UDOM lecturers.
The UDOMASA chairman, Loisulie said Pinda was heading to Dodoma to work on the problems affecting the university.
Loisulie said staff were still on a go-slow attending an endless meeting including planning to file a case in court against UDOM leadership.
On Tuesday this week UDOMASA vowed to maintain their go-slow until they receive satisfactory response from the Treasury or from President Jakaya Kikwete.
The lecturers have been in a continuous meeting since Sunday to press the university authority to pay them new salary rates approved in November last year.
The academicians have vowed not to resume teaching until they meet with president Kikwete to air their grievances.
The UDOMASA chairperson, Paul Loisulie was quoted saying that they have heard that the university management has spoken to the Treasury for clarification on the new salaries.
UDOM Vice Chancellor Prof Kikula said the problem originated from one staff that went to the Treasury to show his/her salary slip being paid more than what the UDOM lecturers are getting.



Saturday 15 January 2011

VURUGU BADO ZARINDIMA UDOM,MKUU WA MKOA NA WILAYA WATEKWA NA WANAFUNZI.........WADAI PROF.MLACHA AJIUZURU..

copyright;maisha blog

Sehenu ya umati wa wanafuzi wakiwa kwenye maandamano UDOM
Habari zilizotufikia mezani jioni hii kutoka katika chuo kkuu cha Dodoma (UDOM) zinathibitisha kuwa mkuu mkoa na wa wilaya ya Dodoma wametekwa na msafara wake na wanafunzi wa chuo cha elimu UDOM, wanafunzi hao walikuwa wakimtaka waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda aje na kumuondoa makamu mkuu wa chuo fedha na utawala Prof.Mlacha.
Wakionekana kuwa  wenye hasira walitoa upepo kwenye rairi za gari za wakuu hao pia kuziba vioo vya gari kwa mabango ili kuzuia msafara huo usiondoke hadi pale Waziri mkuu atakapo toa tamko la kumuondoa Prof. Mlacha ambaye wanaona ndiye kikwazo chuoni hapo.
vijana hao wakiwa wamecharuka kabisa, wanataka mkuu huyo wa fedha mipango na utawala asiendelee na nafasi yake kwani anadharau na majibu ya kejeli kwa wanafunzi na wahadhiri wa UDOM. Akisoma taarifa kwa waziri mkuu, kiongozi wa wanafunzi alimshambulia sana DVC PFA huyo prof. Mlacha na kumtaka kuachia madaraka mara moja ili kupisha maendeleo chuoni hapo.
Waziri mkuu alikitembelea chuo hicho cha Dodoma (UDOM) leo na kuzungukia maeneo mbalimbali chuoni hapo kisha kuahidi kurudi kuongea na baadhi ya makundi kadhaa ya wana UDOM hususani Wanataaluma ambao wapo kwenye mgomo baridi tangu J3 manamo saa saba mchana lakini hakuweza kurudi chuoni hapo na badala yake kutuma ujumbe kupitia kwa wziri wa elimu kuwa hali yake ya kiafya siyo nzuri na hivyo kuahidi kuongea na makundi hayo hapo kesho.

Hali kwasasa bado siyo nzuri sana chuoni hapo kwani kila mmoja angali akiwa na shauku kujua nini Mh.waziri atasema hiyo kesho.
Imeletwa na mwakilishi wa blog hii UDOM
 (D.M)

News update;Waziri mkuu atembelea UDOM!!

Leo waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Mizengo Pinda ametembelea chuo kikuu cha Dodoma maalufu kama UDOM ili kuzungumza na wanafunzi pamoja na wafanya kazi katika kutafuta suruhu ya migogoro inayolindima chuoni hapo kwa takribani wiki mbili sasa. Endelea kuwa nami habari kamili itafuata baadae....

MAHUJAJI ZAIDI YA 100 WAFA AJALINI NCHINI INDIA!!

Habari kutika nchini India zinasema zaidi ya mahujaji 100 wamekufa kwa ajali wakati wakiwa njiani kutokea kwenye ibada yao ya hija maeneo ya milimani kusini mwa jimbo la Keral.
Chanzo cha ajali hiyo kinasemakena kuwa ni kupoteza mwelekeo kwa gari aina ya jeep iliyokuwa imejaza watu ndani yake na hivyo kuseleleka na kuwaangukia mahujaji hao. Kwa mujibu wa taarifa za polisi wamesibitisha kuwa vifo vingi vilisababishwa na mshituko na hivyo kukanyagana na kukosa hewa.Hii ni mara ya pili sasa kutokea kwa majanga katika eneo hilo kwani mwaka 1999 watu zaidi ya 50 walipoteza maisha kutokana na kuporomoka kwa udongo na kuwafunika mahujaji.
Eneo hilo maarufu la sala hutembelewa na watu zaidi ya millioni tatu kila mwaka.



Friday 14 January 2011

WAFANYAKAZI UDOM WASISITIZA KUENDELEZA MGOMO WAO!!



Taarifa zilizoifikia blog yetu mapema hii leo kutoka kwa mwakilishi wetu aliyepo University of Dodoma Tanzania (UDOM) zinasema kuwa bado kuna fukuto kubwa sana la wafanyakazi na wahadhili kutoendela na kazi zao hadi hapo madai yao ya msingi yatakapo timizwa. Wafanyakazi hao ambao wameonyesha hali ya kuchoshwa sana na kauli za uongozi wa chuo ambazo zimekuwa si za matumaini na kutotilia maanani madai yao kwa pamoja wametoa taarifa yao inayoonyesha sababu za msingi za wao kufikia hatua ya kufanya mgomo. Ifuatayo ni taarifa kamili;

TAARIFA YA MATATIZO YANAYOWAKABILI WAFANYAKAZI WANATAALUMA WA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Utangulizi
Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2007 kumekuwa na maendeleo makubwa ya miundo mbinu mbalimbali hasa majengo na barabara. Chuo kimepanuka kwa kiwango cha kuridhisha na hii ni hatua ya kupongezwa na mpenda maendeleo yeyote.

Sanjari na ujenzi wa miundo mbinu kutokana na kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi watumishi wa fani mbalimbali wamekuwa wakiajiriwa tangu kuanzishwa kwa chuo. Katiba ya Chuo (University Charter) imeweka wafanyakazi katika makundi makuu mawili. Moja ni kundi lenye wafanyakazi wanataaluma ambao pamoja na mambo mengine kazi yao kubwa ni ufundishaji, utafiti na ushauri; na pili ni kundi la wafanyakazi wa upande wa utawala. Hata hivyo chuo kinakua kwa haraka sana na hivyo kuhitaji idadi ya wafanyakazi iendanayo na kasi ya ukuaji wa chuo.

Matatizo ya Wafanyakazi  Wanataaluma UDOM
Pamoja na jitihada nzuri ya kuajiri wafanyakazi ili kukidhi mahitaji ya chuo, kumekuwapo matatizo mbalimbali yanayowakabili wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Matatizo makubwa yanaegemea katika swala la malipo ya stahili mbalimbali pamoja na mishahara kama inavyoelekezwa katika nyaraka mbalimbali za serikali. Mkutano wa 4 wa UDOMASA umeainisha matatizo hayo ni kama yafuatavyo:

Mosi, wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma hawajapata mishahara mipya tangu kutangazwa kwa ongezeko la asilimia 20-30 mwezi Julai 2010 kupitia Waraka wa Msajili wa Hazina namba 4, wa mwaka 2010 uliotolewa 3 Agosti 2010. Ushahidi toka Hazina umeonesha kwamba mishahara mipya ililipwa mwezi Novemba 2010 kwa vyuo vikuu vyote vya umma ikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma. Mkutano umeazimia kwamba fedha hizo za mishahara ambayo menejimenti ya UDOM imekata kupitia mishahara mipya ya Hazina zilipwe kwa wahusika mara moja wakati mkutano wa wanataaluma unaendelea.

Pili, Hazina imekuwa ikilipa mishahara ya juu katika ngazi husika lakini menejimenti ya UDOM inapunguza kwa visingizio mbalimbali. Kwa mfano, mfanyakazi mwenye Check No 11818320 (PUTS 15), Hazina mwezi Novemba na December ilimlipa 2,269,890/=, Chuo kilimlipa 1,605,310/= jambo linaloashiria udanganyifu. Payroll ya Hazina inaonesha kuwa fedha inayotoka hazina ni tofauti na fedha anayolipwa mwanataaluma hapa UDOM. Wanataaluma wana wasiwasi kuwa tabia hii ya kupunguza mishahara imekuwa ikiendelea kwa muda sasa. Hivyo, mkutano umeazimia kuwa fedha zote ambayo menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imekuwa ikikata zilipwe.

Tatu, upunguzwaji wa mishahara inayotoka Hazina kimsingi umeathiri uchangiaji wetu katika mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF, LAPF, PPF, PSPF n.k.), pamoja na michango yetu katika vyama vya wafanyakazi kama vile RAAWU. Hali hii ya upunguzwaji mishahara pia umeathiri uchangiaji wa mwajiri katika mifuko ya hifadhi ya jamii kama inavyotakiwa na sheria husika. Mfano mfanyakazi anayelipwa 853,300/= badala ya 1,248,070/= kama ilivyo katika payroll ya hazina anachangia LAPF kiasi cha 42,665/= (asilimia 5) kwa mwezi badala ya 62,403.3/= kwa mwezi. Pia uchangiaji wa mwajiri unapungua hali ambayo itaathiri mafao ya uzeeni. Mkutano umeazimia kuwa kiasi chochote ambacho kilipunjwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na vyama vya wafanyakazi ilipwe mara moja wakati wanataaluma wanaendelea na mkutano wao.

Nne, Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikitoa salary slips zake badala ya kutoa salary slips zinazotka Hazina. Aidha menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imedai kuwa Hazina haitoi salary slips. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na uongozi wa UDOMASA umeonesha kuwa salary slips zimekuwa zikichukuliwa kutoka hazina na maafisa wa UDOM. Madai ya menejimenti ya UDOM kuwa hazina haitoi salary slips yanaashiria mbinu inayotumiwa kupunja mishahara ya wafanyakazi inayotoka Hazina. Mkutano umeazimia kuwa kila mfanyakazi apatiwe salary slips zake tangu Hazina waanze kutoa.

Tano, fedha za kujikimu wakati wa kuanza ajira pamoja na usafirishaji wa mizigo wakati wa kuja kuanza kazi hatujalipwa. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imeripotiwa mwaka 2008 ikisema kuwa zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi wa taasisi hii hawakustahili kulipwa fedha za kujikimu. Mazungumzo ya hivi karibuni yamepelekea menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma kukubali kuwa fedha za kujikimu ni stahili ya mfanyakazi yeyote anapoanza kazi, ingawa wamesema kinagaubaga kuwa haitaweza kulipa stahili hizo kwa sasa kwa kisingizio kuwa ni fedha nyingi sana. Mkutano umeazimia kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kilipe stahili hizi kwa wafanyakazi wote. Zoezi hili la malipo ya fedha ya kujikimu lifanyike mara moja wakati wanataaluma wakiendelea na mkutano wao.

Sita, katika kikao cha tarehe 29 Desemba, 2010 kati ya menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma na viongozi wa UDOMASA iliripotiwa na menejimenti ya chuo kuwa wafanyakazi 409 hawajasajiliwa katika payroll ya Hazina. Aidha menejimenti imeshindwa kutoa sababu za msingi kwa tatizo hili licha ya kuwa wafanyakazi hao wameshafanya kazi kwa miezi kadhaa sasa. Mkurugenzi wa Rasilimaili Watu katika Chuo hiki alitoa sababu zisizoweza kuaminika kuwa Hazina ndiyo yenye matatizo. Aidha, uongozi wa UDOMASA imeuliza swala hili Hazina lakini lawama zilirudishwa menejimenti ya UDOM. Hali hii ya kutoingizwa wafanyakazi katika Payroll ya Hazina, pamoja na mambo mengine unapelekea wafanyakazi wa UDOM kuishi kwa mashaka makubwa kwa kuwa menejimenti ya UDOM imekuwa ikitenda kazi zake si kwa kuzingatia kanuni bali kwa vitisho. Mkutano umetoa umeazimia kuwa wafanyakazi wote ambao mpaka sasa walikuwa hawajaingizwa kwenye payroll ya Hazina wawe wameingizwa ifikapo mwisho wa mwezi Januari, 2011. Aidha, ofisi iliyohusika na uzembe huu ndani au nje ya menejimenti ya UDOM iwajibike.

Saba, Chuo Kikuu cha Dodoma kimeandaa Sera ya Mazishi ambayo inafanya mwajiri kukwepa wajibu wake wa kisheria. Menejimenti ya UDOM kwa miezi kadhaa sasa imekuwa ikikata 3,000/= kwa wafanyakazi kila mwezi bila idhini ya waajiriwa. Na uwajibikaji wa fedha haupo wazi. Hali hii inaashiria kuwa menejimenti ya chuo inafanya kazi nje ya kanuni na sheria zinazosimamia makato ya fedha. Mkutano umeazimia kuwa chuo kisimamishe ukataji huo na timu huru iundwe na isimamie fedha hizo, wakati wadau wakifanya mchakato wa kuijadili upya kuhakikisha inakidhi mahitaji yao, na mwajiri hakwepi jukumu lake.

Nane, lingine ni kutokuwepo kwa samani katika ofisi za wanataaluma na wengine hawana ofisi kabisa. Tatizo hili la samani na vitendea kazi vingine limefanya mazingira ya kazi kuwa magumu mno kwa utendaji wa wanataaluma kama vile ufundishaji na pia wanafunzi wameathirika kwa kuwa wanawakosa walimu wao maofisini. Vitendea kazi kama vile kompyuta na printer zipo katika baadhi ya ofisi ya wakuu wa idara pekee. Pia ukubwa wa madarasa unaadhiri utendaji wa walimu kwa kuwa baadhi ya madarasa yana idadi kubwa ya wanafunzi (mfano zaidi ya 1200 katika ukumbi mmoja). Mkutano umeazimia kuwa wanataaluma wote wapatiwe ofisi zenye samani (meza, viti, makabati, dustbin n.k), pamoja na vitendea kazi vingine kama kompyuta, projector ili kuweza kurahisisha mazingira ya kazi.


Juhudi zilizofanywa na UDOMASA kutatua matatizo tajwa
Matatizo yaliyoanishwa hapo juu ni ya msingi na yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa chuo mwaka 2007. Jumuiya ya wanatalaamu (UDOMASA) imefanya juhudi mbalimbali bila mafanikio. Juhudi hizo ni kama ifuatavyo

Tarehe 17 Novemba, 2008 ulifanyika mkutano mkuu wa kwanza wa UDOMASA kwa ajili ya kujadili mambo ya msingi likiwemo suala la fedha za kujikimu. Jambo hili lilijadiliwa tena katika mkutano mkuu wa pili tarehe 18 Novemba, 2008. Pamoja na juhudi za uongozi wa UDOMASA kuongea na menejimenti ya chuo walijibiwa kuwa asilimia kubwa ya waajiriwa UDOM hawastahili fedha za kujikimu. Hali hii ilipelekea wanataaluma kugoma kufanya kazi, na baadaye wanataaluma watatu kusimamishwa kazi kwa kisingizio cha kuchochea mgomo huo. Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Dr Kisanga, Titus Mpemba, na Rajab Chipila. Kutokana na kusimamishwa kwa wanataaluma hao umoja wao uliyumbishwa au kusambaratishwa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja hadi hali ya umoja ilipofufuka mwishoni mwa mwaka jana, 2010 baada ya uongozi wa kwanza wa UDOMASA kumaliza muda wake kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe 19 Oktoba, 2010.

Tarehe 10 Novemba, 2010 uongozi mpya UDOMASA ulikwenda kuonana na menejimenti ya UDOM kwa ajili ya utambulisho lakini menejimenti ikawakataa kwa kisingizio kuwa hawakuwa na sifa za wanataaluma. Hata hivyo viongozi wapya wa UDOMASA waliiambia menejimenti ya UDOM kuwa wapo tayari kuachia ngazi iwapo menejimenti itatoa barua kueleza kutowatambua na kuthibitisha si wanataaluma, jambo ambalo halikutekelezwa. Siku chache baadaye mwenyekiti mpya wa UDOMASA, Paul Loisulie, alipokea barua kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo ambayo ilishauri kuwa viongozi wapya wa UDOMASA wanatakiwa kutumia muda mwingi ili kujiendeleza kimasomo na si kujiingiza katika siasa za UDOMASA. Barua hii ambayo kimsingi haikurejea kauli ya Makamu Mkuu wa Chuo ya kuwa viongozi wapya wa UDOMASA hawakuwa na sifa zinazotakiwa ilitafsiriwa na wana UDOMASA kuwa ni dhamira ya chuo kudhoofisha umoja wa wanataaluma hapa chuoni.

Baada ya muda si mrefu uongozi mpya wa UDOMASA uliomba kibali cha mkutano mkuu kutoka kwa DVC-PFA na kukubaliwa. Hivyo mkutano mkuu wa tatu ukafanyika tarehe 4 Desemba 2010 ambao pamoja ulijadili fedha za kujikimu, mishahara mipya kama inavyoelekezwa na waraka wa Hazina namba 4, 2010, na sera ya mazishi. Mkutano uliamua kuwa viongozi wa UDOMASA wafanye uchunguzi wa kinachoendelea kwa masuala ya fedha ya kujikimu na mishahara mipya.

Ufuatiliaji ulifanyika kwa kwenda Ofisi ya Utumishi wa Umma; Hazina; na Wizara ya Elimu. Hazina ilikiri kuwa mishahara mipya ilishapelekwa katika vyuo vikuu vyote kikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma. Aidha, Hazina iliongeza kuwa fedha ya kujikimu inatakiwa kulipwa kupitia Other Charges (OC) ya taasisi husika, kwa hiyo UDOM pia ilitakiwa kulipa fedha ya kujikimu kupitia OC.

Viongozi wa UDOMASA walipokwenda Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma waliambiwa kuwa ofisi hiyo inahusika na sera na kwamba masuala ya taasisi za umma yanashughulikiwa na Msajili wa Hazina. Wakaahidi kuwa wangetafuta utaratibu wa kuzungumza na Hazina. Jitihada za kuonana na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu hazikuzaa matunda kwa kuwa wahusika hawakuwepo.

Baada ya kurudi kutoka katika ofisi za juu, uongozi wa UDOMASA ulifanya jitihada kuonana na Msaidizi wa Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) na Mkurugenzi wa rasilimali watu UDOM ambao walidai kuwa mishahara mipya imeletwa lakini ilikuwa na makosa makubwa. Pia walikiri kuwa fedha ya kujikimu zinatakiwa kutoka ndani ya chuo (OC) lakini ikadaiwa kuwa fedha hazitoshi kulipa wafanyakazi kwa kuwa ni wengi sana kwa sasa.

Tarehe 29 Desemba, 2010 uongozi wa UDOMASA ulikutana na menejimenti ya UDOM ambapo taarifa ya mishahara kuanzia 2007 hadi Novemba 2010 ilisomwa na Mkurugenzi wa rasilimali watu. Pia iliripotiwa kuwa wafanyakazi 409 hawakuwapo katika payroll ya hazina. Menejimenti ya chuo ilitoa lawama kwa hazina kwa matatizo yanayohusiana na mishahara, fedha ya kujikimu pamoja na wafanyakazi 409 kutokuwapo katika orodha ya hazina. Hivyo, baada ya majadiliano kikao kiliunda timu ya watu watano (Mkurugenzi rasilimali watu, Msarifu, Wawakilishi wawili wa UDOMASA, na mwakilishi mmoja wa RAAWU) ili kuweza kufuatilia matatizo hayo. Pia ilikubaliwa kuwa fomu ziletwe ili ziweze kujazwa na wafanyakazi ambao hawapo katika payroll ya hazina ili timu iweze kwenda nazo wiki ifuatayo. Aidha, ilikubaliwa pia Makamu Mkuu wa Chuo asionane na wafanyakazi kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya mpaka hapo timu itaporudi kutoka Dar es Salaam.

Kinyume na makubaliano, Mkurugenzi rasilimali watu pamoja na Msarifu walikwenda Dar es Salaam siku iliyofuata hali ambayo iliwapa taabu viongozi wa UDOMASA pamoja na wafanyakazi kwa ujumla. Kutokana na hili viongozi wa UDOMASA walikwenda kumuuliza Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) kuhusu safari ya ghafla ya watu waliotakiwa kuwa katika timu ya kufuatilia matatizo, lakini alieleza kuwa safari ile ilikuwa ya mambo ya bajeti. Tuliamini kimsingi, bila ushahidi wowote.

Mwenyekiti na Katibu wa UDOMASA pamoja na Mwenyekiti wa RAAWU tawi la UDOM waliweza kuondoka tarehe 4, Januari 2011 kwenda Dar es Salaam kuungana na Msarifu na Mkurugenzi rasilimali watu kwa ajili ya kutatua matatizo yanayowakabili wafanyakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha tarehe 29 Desemba, 2011.

Wakati tunaendelea kusubiri majibu kutoka timu iliyokwenda Dar es Salaam tuliona matangazo yaliyobandikwa katika mbao mbalimbali za matangazo yakidai kuwa Makamu Mkuu wa Chuo alitaka kuongea na wafanyakazi tarehe 6 Januari, 2011 saa nane mchana. Mkutano huu wa Makamu Mkuu wa Chuo na wafanyakazi ulikwenda kinyume na makubaliano ya kikao cha tarehe 29 Desemba, 2010. Hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo alipomaliza kutoa taarifa katika mkutano wake na wafanyakazi, Makamu Mwenyekiti wa UDOMASA alimtaka ajibu madai ya msingi ya wafanyakazi (fedha za kujikimu, mishahara mipya) kwa kuwa alifanya mkutano kinyume na makubaliano. Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo pia alitakiwa kueleza habari zilizozagaa kuwa chuo kililetewa mishahara mipya kuanzia Novemba, 2010 lakini chuo hakikuwa tayari kulipa kama ilivyoletwa kutoka hazina. Makamu Mkuu wa Chuo hakuweza kujibu. Aidha, katika mkutano wa Makamu Mkuu wa Chuo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) alieleza kuwa amepokea barua ikimshauri kuanza kupunguza deni la fedha ya kujikimu kupitia OC.

Tarehe 8 Januari, 2011 wanataaluma walifanya mkutano mkuu wa nne ikiwa pamoja na mambo mengine kupokea taarifa ya maswala muhimu ya stahili za wafanyakazi. Baada ya kujadiliana kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni mkutano uliahirishwa kwa masharti ya kuendelea siku ya Jumatatu ya tarehe 10 Januari, 2011.

Hitimisho
Kwa kuwa uongozi wa UDOMASA umefanya jitihada za kufuatilia utatuzi wa matatizo haya yanayohusiana na fedha katika Hazina; Wizara ya Elimu; na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na kuonekana kuwa matatizo yapo hapa ndani ya chuo; na kuwa menejimenti ya UDOM mpaka wanataaluma wanakwenda kwenye mkutano haikuwa tayari kushughulikia matatizo haya, Mkutano Mkuu wa nne wa UDOMASA wa tarehe 8 Januari, 2011 uliamua umwombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aingilie kati suala hili. Pia wanataaluma wameamua kuendelea kufanya mikutano mpaka hapo matatizo yatakapopatiwa ufumbuzi.
 Imetolewa na Paul Loisulie
Mwenyekiti UDOMASA


Thursday 13 January 2011

Tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Juu ya Mauaji ya Wananchi wakati wa Maandamano ya Amani yaliyofanyika Arusha tarehe 5 Jan, 2011


UTANGULIZI
Tumekutana hapa leo hii kwa huzuni kubwa. Tumekutana hapa leo hii kwa sababu watoto wa familia mbili wamepoteza baba zao na mama wa familia hizo wamepoteza waume na wenzi wao wa maisha. Tumekutana hapa leo kwa sababu wazazi wa familia mbili wamepotelewa na watoto wao wa kiume. Tumekutana hapa leo kwa sababu kuna familia nyingine – kwa sababu taarifa zetu za awali zinaonyesha watu wengine zaidi wameuawa - zimepotelewa na wapendwa wao vile vile.
Tumekutana hapa leo kwa sababu mamia ya wananchi wa Jiji hili wameumizwa kwa kupigwa risasi za moto, kupigwa mabomu ya machozi na/au kupigwa kwa virungu na mabuti ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Tumekutana hapa leo kwa sababu wote waliokufa na tunaowaomboleza leo na wote walioumizwa na/au kuharibiwa mali zao hawakufikwa na mauti na/au majanga hayo kwa ajali ya barabarani au tetemeko la ardhi. Tumekutana hapa kwa sababu wote waliofikwa na mauti wameuawa na wote walioumia wameumizwa na Jeshi la Polisi la Tanzania.
Tumekutana hapa leo kwa sababu Jeshi la Polisi la Tanzania halipaswi, na halikupaswa, kuua wananchi wasiokuwa na hatia yoyote na ambao walikuwa wanatumia haki yao ya kufanya maandamano ya amani inayotambuliwa na Katiba na sheria za nchi yetu. Na tumekutana hapa leo ili kulinda na kutetea haki hiyo na kuzuia nchi yetu kuwa dola ya kipolisi inayoendeshwa kwa amri za kijeshi na za watawala na sio kwa matakwa ya wananchi.
Lakini, ndugu wananchi wa Arusha, tumekutana hapa ili kuomboleza kwa pamoja na tunahitaji kuomboleza kwa amani. Kwenye msiba watu hawapigani na tunawaomba tusipigane kwenye msiba huu. Kwenye msiba watu hawafanyi fujo na tunawaomba tusifanye fujo kwenye msiba huu. Tunawaomba tuomboleze kwa amani ili tusiwape wale walioua ndugu zetu sababu ya kusema kwamba sisi tunapenda fujo na uvunjifu wa amani.

SIKU YA KIHISTORIA
Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Jiji la Arusha. Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Tanzania. Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania – ambalo limepewa wajibu wa kisheria wa ‘kulinda amani, sheria na utulivu, kugundua na kuzuia uhalifu, kukamata na kudhibiti wahalifu na kulinda mali za wananchi – liliamua kwa makusudi kuacha kutimiza wajibu wake kisheria na kujipa wajibu mwingine wa kuwa ni Jeshi la kuvunja amani, kukiuka sheria, kuvuruga utulivu, kufanya uhalifu na kuharibu mali za wananchi. Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania – ambalo limejipachika kauli mbiu ya ‘Ulinzi wa Raia na Mali Zao’ – liliamua kwa makusudi kubadili kauli mbiu yake kuwa ni ‘Mauaji ya Raia na uharibifu wa mali zao’!
Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo wananchi wa Jiji la Arusha walivamiwa kwa makusudi, waliuawa kikatili na kupigwa na kuumizwa bila kosa au sababu yoyote ya msingi. Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania lilitumia silaha kubwa kubwa – risasi za moto, mabomu ya machozi na magari ya maji ya kuwasha – dhidi ya raia waliokuwa na vitambaa vyeupe vyenye kuashiria amani. Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo – kama ilivyokuwa tarehe 26 na 27 Januari 2001 – Jeshi la Polisi la Tanzania lilitukumbusha tena kwamba liko tayari kumwaga damu ya Watanzania wasiokuwa na hatia ili kulinda wizi wa kura na unyongaji wa demokrasia unaofanywa na watawala wa Chama cha Mapinduzi.
Kama ilivyokuwa Zanzibar miaka kumi iliyopita ndivyo ambavyo imekuwa Arusha mwaka huu: tumeanza Mwaka Mpya kwa umwagaji wa damu na maombolezo badala ya sherehe na kutakiana heri! Hata hivyo, tofauti na ilivyokuwa Zanzibar baada ya mauaji ya Januari 2001, CHADEMA haitakubali kununuliwa au kunyamazishwa kwa kuvikwa vilemba vya ukoka na/au kupewa vipande thelathini vya fedha ili kunyamazia mauaji ya wananchi wetu: Mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia hayatazuia jitihada za kujikomboa kutoka kwenye makucha ya utawala wa CCM. Mti wa haki uliorutubishwa kwa damu isiyokuwa na hatia ya wananchi wa Arusha utaendelea kukua na kuenea Tanzania nzima. Tarehe 5 Januari 2011 itakuwa siku itakayokumbukwa katika historia ya nchi yetu kama ni siku ambayo jitihada za ukombozi wa nchi yetu zilipata msukumo mkubwa.

MAANDAMANO HALALI
Jeshi la Polisi lilijua kwamba kutakuwa na maandamano ya amani ambayo yangefuatiwa na mkutano wa hadhara. Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu njia na/au barabara za Jiji la Arusha ambazo maandano hayo ya amani yangepitia hadi kufika kwenye eneo la Viwanja vya NMC ambako mkutano wa hadhara ungefanyika. Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu muda wa kuanza maandamano hayo ya amani na muda wa kumalizika kwa mkutano wa hadhara.
Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu yote hayo sio kwa sababu ya ‘taarifa za kiintelijensia’ ambayo ndio imekuwa kisingizio cha Jeshi la Polisi la Tanzania kukanyaga haki za kikatiba za wananchi wa Tanzania kupinga serikali ya CCM kwa njia za amani kwa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara. Jeshi la Polisi la Tanzania lilifahamu yote hayo kwa sababu Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilifuata taratibu zote za kisheria za kufanya maandamano na mikutano ya hadhara. Tarehe 3 Januari 2011 CHADEMA ilitoa taarifa ya maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha kuhusu nia yake ya kufanya maandano ya amani yatakayofuatiwa na mkutano wa hadhara ili kupinga kitendo cha watawala wa CCM kuwalazimishia wananchi wa Jiji la Arusha Meya ya Jiji kwa njia za kiharamia.
Tarehe hiyo hiyo Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha alifanya kikao na viongozi wa CHADEMA kwa lengo la kukubaliana njia na/au barabara zitakazotumiwa na waandamanaji hadi kufikia Viwanja vya NMC. Baada ya hapo, pamoja na kwamba hakuwa na haja ya kisheria ya kufanya hivyo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha aliifahamisha CHADEMA kwa maandishi kwamba maandamano yetu ya amani na mkutano wa hadhara yalikuwa yameruhusiwa na Jeshi la Polisi la Tanzania. Hatua zote tulizozichukua na ambazo tumezitaja hapa zilifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na vile vile kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Lakini hata kabla ya hapo, Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajua kwamba CHADEMA ingefanya maandamano ya amani kushinikiza utekelezaji wa madai yetu tuliyoyatoa kwa maandishi kwa serikali na nakala yake kupatiwa Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema mnamo tarehe 23 Desemba 2010. Katika barua yake, CHADEMA ilidai kwamba uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ufutwe na kurudiwa; Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Jiji afukuzwe kazi kwa kushiriki katika ukiukwaji wa sheria za uchaguzi wa viongozi wa halmashauri za serikali za mitaa; na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha avuliwe madaraka yake kwa kushiriki kumpiga Mbunge wetu wa Jimbo la Arusha Mjini aliyekuwa anajaribu kutetea sheria za nchi yetu za uchaguzi wa viongozi wa halmashauri za serikali za mitaa.
CHADEMA ilitoa nafasi ya wiki mbili kwa serikali kutekeleza madai hayo la sivyo ingeandaa maandamano ya amani ya wananchi wa Arusha. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba CHADEMA haikukimbilia kuandaa maandamano hata kama haikuwa kosa dhidi ya sheria za Tanzania kufanya hivyo. Kabla ya matukio ya maandamano ya tarehe 5 Januari, CHADEMA ilishaweka wazi utayari wake wa kumaliza mgogoro wa Arusha kwa njia za mazungumzo. Barua yetu ya tarehe 23 Desemba 2010 kwa serikali na kwa Jeshi la Polisi la Tanzania haijajibiwa hadi leo hii!

JESHI LA WAHALIFU!
Baada ya taarifa ya maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA kutolewa kwa mujibu wa sheria zilizotajwa, njia pekee halali ya kusitisha maandamano na mkutano uliopangwa ilikuwa ni kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha kutoa amri ya kusitisha maandamano na mkutano huo. Na Sheria ya Jeshi la Polisi inasema wazi kwamba Ofisa wa Polisi aliyepewa taarifa ya maandamano au mkutano hatatoa amri ya kuzuia au kusitisha maandamano au mkutano huo ‘isipokuwa tu kama amejiridhisha kwamba maandamano au mkutano huo unaweza kusababisha uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama na/au utulivu wa umma au kutumiwa kwa malengo haramu.’
Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, chama cha siasa kikishatoa taarifa ya mkutano kinaruhusiwa kufanya mkutano huo isipokuwa tu na kama kitapokea amri kutoka kwa ofisa wa polisi mwenye mamlaka ya eneo husika ikielekeza kwamba mkutano huo usifanyike kama ilivyopangwa. Na chini ya sheria hii vile vile, ofisa wa polisi aliyepewa taarifa ya mkutano haruhusiwi kutoa amri ya kuzuia au kusitisha maandamano au mkutano huo mpaka atakapojiridhisha kwamba mkutano au maandamano hayo yana lengo la kutekeleza au kutumiwa kwa malengo haramu; au kama maandamano au mkutano huo unaweza au umelenga kusababisha uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama na/au utulivu wa umma katika eneo husika. Kwa vyovyote vile kwa mujibu wa sheria hizi mbili, amri ya kuzuia na/au kusitisha maandamano au mkutano wa hadhara uliotolewa taarifa ni lazima iwe ni ya maandishi.
Na hata kama ‘taarifa za kiintelijensia’ alizozisema Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema zilikuwa na ukweli - kwamba kulikuwa na uwezekano wa uvunjifu wa amani iwapo maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA ungeendelea kama ilivyokuwa imepangwa - bado Jeshi la Polisi la Tanzania lisingepaswa kutoa amri ya kuzuia na/au kusitisha maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA. Hii ni kwa sababu, kuzuia na/au kusitisha maandamano sio hatua pekee inayoweza kuchukuliwa na Jeshi la Polisi la Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kila chama ambacho kimesajiliwa ‘kina haki ya kupatiwa ulinzi na msaada wa vyombo vya ulinzi kwa malengo ya kuwezesha mikutano yenye amani na utulivu.’
Jeshi la Polisi la Tanzania lilikiuka kwa makusudi masharti haya ya sheria. Kwanza, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha ambaye ndiye ofisa anayetakiwa kupatiwa taarifa ya maandamano na mkutano wa hadhara hakuwahi kuipa CHADEMA taarifa yoyote ya maandishi ya kuzuia na/au kusitisha maandamano na mkutano wa hadhara uliotolewa taarifa rasmi kwake kwa mujibu wa sheria. Taarifa na/au amri pekee tunayoisikia ya kuzuia na/au kusitisha maandamano ni ile inayosemekana ilitolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha jioni ya tarehe 4 Januari 2011. Taarifa na/au amri hiyo – kama kweli ilikuwepo - ilikuwa ni haramu kwa sababu Kamanda wa Polisi wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuruhusu au kukataza maandamano na/au mikutano ya vyama vya siasa. Mtu pekee mwenye mamlaka hayo chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa ni ‘ofisa polisi mwenye mamlaka ya eneo’ la mkutano, kwa maana nyingine, Mkuu wa Polisi wa Wilaya!
Aidha, tuna taarifa kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema alitangaza kwenye vyombo vya habari kwamba maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA yamepigwa marufuku kutokana na kuwepo kwa ‘taarifa za kiintelijensia’ kwamba kutakuwa na uvunjifu wa amani wakati wa maandamano na/au mkutano huo wa hadhara. Tangazo hilo la Inspekta Jenerali wa Polisi lilikuwa haramu na ni ukiukaji wa makusudi wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa kwa sababu Inspekta Jenerali wa Polisi hana mamlaka yoyote kisheria ya kuzuia au kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Vile vile utaratibu wa kutoa amri za kuzuia ama kusitisha maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwa kutumia matangazo ya televisheni na/au waandishi wa habari ni utaratibu mgeni katika nchi ya Tanzania na hautambuliwi kabisa na sheria hizo!
Lakini hata kama maandamano na mkutano wetu wa hadhara yangekuwa yamepigwa marufuku kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa – kitu ambacho hakikufanyika – bado CHADEMA ilikuwa na uhalali wa kuendelea na maandamano hayo na kufanya mkutano kama ilivyopangwa. Hii ni kwa sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kulinda uhuru wa wananchi ‘kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani….’ Hii ina maana kwamba uhuru wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara umepanuliwa sana na hauwezi kupokonywa kihalali kwa visingizio vya ‘taarifa za kiintelijensia’ vya Jeshi la Polisi la Tanzania.
Kwa hiyo wananchi wa Arusha walivamiwa na kupigwa risasi zilizowaua au kuwajeruhi sio kwa sababu walikuwa wamevunja sheria yoyote ya Tanzania. Walivamiwa na kuuawa au kujeruhiwa na mali zao kuharibiwa sio kwa sababu walifanya kosa lolote linalotambuliwa na sheria za nchi yetu. Viongozi wa CHADEMA kuanzia ngazi za juu za kitaifa hadi ngazi za chini na wanachama wetu wa kawaida walishambuliwa kwa risasi na mabomu na baadaye kujazwa kwenye mahabusu za polisi sio kwa sababu walikiuka sheria yoyote. Wananchi wa Arusha walifanyiwa uhalifu wote huo licha ya kwamba Katiba ya nchi yetu inatambua na kulinda uhuru wa wananchi wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara.

MAUAJI YA KUPANGWA
Mauaji ya Arusha yalifanywa kwa makusudi na kwa kupangwa. Jeshi la Polisi la Tanzania lilipanga na kutekeleza mauaji hayo. Lakini sio Jeshi la Polisi la Tanzania pekee lenye kuhusika na mauaji ya wananchi wetu. Rais Kikwete na serikali yake na chama chake cha CCM wanahusika moja kwa moja na damu iliyomwagwa kwa makusudi Arusha. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama. Aidha, chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi – ambaye ni mteuliwa wa Rais – anawajibika kufuata amri na maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani – mteuliwa mwingine wa Rais – kuhusiana na udhibiti wa shughuli za Jeshi la Polisi. Kwa hiyo, kikatiba na kisheria, Jeshi la Polisi liko chini ya mamlaka ya Rais na wateuliwa wake kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Inspekta Jenerali wa Polisi.
Pamoja na mamlaka ya Rais juu ya Jeshi la Polisi, Kikwete mwenyewe alikwishatoa kauli na matamko hadharani ambayo yaliashiria kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajiandaa kumwaga damu ya Watanzania ili kulinda utawala wake na wa chama chake. Kwa mfano, katika hotuba yake ya Mwaka Mpya aliyoitoa usiku wa tarehe 31 Desemba 2010, Kikwete alidai kwamba ‘… wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa … wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara…. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili.’ Katiba hotuba hiyo, Kikwete alizungumzia kile alichokiita wananchi ‘kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara’!
Rais aliyasema hayo wiki moja baada ya barua yetu kwa serikali yake juu ya nia ya CHADEMA kufanya maandamano ya amani iwapo serikali yake isingechukua hatua tulizodai zichukuliwe katika barua yetu ya tarehe 23 Desemba 2010. Haikupita hata wiki moja tangu Kikwete atoe kauli yake hiyo na Jeshi la Polisi la Tanzania limemwaga damu ya Watanzania Arusha. Jeshi la Polisi la Tanzania limetekeleza maagizo ya Amiri Jeshi wake mkuu, ndio maana Amiri Jeshi Mkuu huyo hajatoa kauli yoyote kwa Watanzania kuhusiana na matukio haya ya kusikitisha na wala kuchukua hatua kuwawajibisha wale waliotoa amri za kuua na kuumiza Watanzania na/au waliozitekeleza

KISASI CHA UCHAGUZI MKUU!
Mauaji ya wananchi wetu, matumizi ya nguvu ya kutisha dhidi ya wanawake, watoto na wazee na kukamatwa kwa mamia ya viongozi, wanachama na wananchi wa kawaida wa Jiji la Arusha ilikuwa ni kulipa kisasi kwa viongozi wa CHADEMA wa ngazi zote na kwa wananchi wa Arusha kwa kudiriki kuisambaratisha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania lilidiriki kumvamia na kumpiga Mbunge wetu wa Arusha Mjini hadi akapoteza fahamu wakati alipojaribu kulinda haki ya wananchi wa Arusha kuwa na Meya wa Jiji wanayemtaka na sio anayetakiwa na mafisadi wa nchi hii na chama chao.
Jeshi la Polisi la Tanzania limelipa kisasi kwa niaba ya CCM kwa sababu wananchi wa Arusha wamediriki kutumia haki zao za kisheria kupinga mipango ya mafisadi kuingiza Meya wa Jiji la Arusha atakayelinda maslahi ya mafisadi na chama chao. Wananchi wa Arusha wamelipiziwa kisasi na Jeshi la Polisi la Tanzania kwa sababu mafisadi wanajua wangeruhusu haki itendeke katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha CCM ingesambaratishwa kama ilivyosambaratishwa katika Uchaguzi Mkuu.
Mauaji ya Arusha sio kisasi cha CCM dhidi wananchi wa Arusha tu. Ni kisasi pia dhidi ya wananchi wa Tanzania na dhidi ya CHADEMA. Ni kisasi dhidi ya Watanzania wote kwa sababu, kwa mara kwanza tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa urudishwe mwaka 1992, Uchaguzi Mkuu wa 2010 ulionyesha wazi kwamba CCM imeanza safari yake ya mwisho kuelekea kwenye jaa la taka taka la historia. Kwa mara ya kwanza, CCM ilipoteza miji mikubwa karibu yote ya Tanzania. Licha ya uchakachuaji wa kura, rushwa na uharamia wa kutisha, CCM imepoteza Jiji la Dar es Salaam, Jiji la Mwanza, Jiji la Arusha, Jiji la Mbeya na miji mikubwa kama vile Moshi, Iringa na Musoma.
Lakini CCM na mafisadi hawakupoteza miji tu, wamepoteza pia majimbo ya vijijini. CCM imepoteza nusu ya Shinyanga, zaidi ya nusu ya Kigoma, sehemu kubwa za Manyara, Singida, Mbeya, Iringa na mikoa mingine ambayo kihistoria imekuwa inaonekana kama ngome za CCM. Na licha ya nguvu nyingi za dola na za fedha za ufisadi, Jakaya Kikwete amepunguza idadi ya kura zake kutoka kura zaidi ya milioni nane alizopata wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 hadi kura milioni tano za mwaka jana, ikiwa ni pungufu ya zaidi ya kura milioni tatu na anguko la asilimia 20!
Kuporomoka kwa CCM kumeenda sambamba na kukua na kuongezeka kwa nguvu ya CHADEMA. Licha ya uchakachuaji wa kura wa kutisha, matumizi ya vyombo vya dola na rushwa ya kutisha, nguvu na ushawishi wa CHADEMA imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Ndio chama cha upinzani chenye Wabunge wengi kuliko vyama vingine vyote vya upinzani kwa pamoja. Ndio chama pekee cha upinzani kilichowahi kupata Wabunge kutoka kanda zote za Tanzania Bara na Visiwani. Ndio chama cha upinzani pekee kilichowahi kupata zaidi ya robo ya kura zote za Rais na Wabunge. Na ndio chama pekee chenye kubeba matumaini ya wananchi wa Tanzania kwamba Tanzania bila ufisadi wa CCM inawezekana. Ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania limelipizia kisasi cha CCM kwa wananchi wa Arusha na viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA

HAKI LAZIMA ITENDEKE ARUSHA!
Damu iliyomwagwa Arusha inalilia haki. Roho za wote waliotolewa muhanga na Jeshi la Polisi la Tanzania zinahitaji haki ili ziweze kutulia na mizimu yao ipumzike. Wote walioumizwa na ujambazi wa Jeshi la Polisi la Tanzania wanalilia fidia ili waweze kuuguza maumivu yao ya kimwili, ya kiroho na ya mali zao zilizoharibiwa. Sheria za nchi yetu zilizokanyagwa chini kana kwamba hazipo zinahitaji kulindwa, kutetewa na kuheshimiwa ili iwe fundisho kwa wahalifu wengine wa aina hii.
Kwa hiyo, sisi wote tuliokusanyika hapa leo, na wale wote wanaotusikiliza mahali popote nchini na hata nje ya nchi yetu, tuna jukumu la kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa wale ambao tunaomboleza vifo vyao hapa leo. Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa wale wote walioumizwa kwa risasi na mabomu na virungu na mabuti ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Tuna jukumu la kuhakikisha wale wote ambao waliharibiwa mali zao kwa sababu ya uhalifu huu wa Jeshi la Polisi la Tanzania wanafidiwa kwa kiasi chote cha hasara waliyoipata. Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania halirudii tena ujambazi wa aina hii dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyote kwa kuwawajibisha wale wote walioshiriki katika ujambazi huu kwa kutoa amri za kuua au kuumiza wananchi na/au kwa kuzitekeleza.
Ili tutimize majukumu yote haya, tunahitaji kuhakikisha kwamba mambo yafuatayo yanafanyika:
  1. Serikali hii iwajibike kwa wananchi kama ilivyotamkwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Waziri wa Mambo ya Nchi Shamsa Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema wajiuzulu mara moja ili kuwawajibisha kama viongozi na wasimamizi wa juu kabisa wa Jeshi la Polisi la Tanzania. Aidha, kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi wetu kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia mengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai;
  2.  Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia;
  3. Fidia stahili ilipwe kwa mujibu wa sheria husika za nchi kwa ndugu na/au jamaa wa wale wote waliouawa kutokana na vitendo vya Jeshi la Polisi la Tanzania na kwa wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile na/au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo;
  4. Mashtaka ya uongo ya jinai yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA, wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi la Tanzania yafutwe bila masharti yoyote kwa sababu maandamano na mkutano wa hadhara uliozuiliwa yalikuwa halali kwa mujibu wa sheria husika za nchi yetu. Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana kesi iliyofunguliwa dhidi yao hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani;
  5. Kwa vile uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndio chanzo cha mauaji ya wananchi na kwa kufahamu utaratibu haramu uliotumika kumpata Meya wa Jiji hilo, matokeo ya uchaguzi huo yafutiliwe mbali na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo kwa kufuata sheria husika za nchi yetu;
  6. Haki ya vyama vya siasa na wananchi kufanya maandamano ya amani kama inavyotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iheshimiwe na kutiliwa nguvu zaidi kwa kufuta vifungu vya Sheria ya Jeshi la Polisi nay a Vyama vya Siasa vinavyoruhusu Jeshi la Polisi la Tanzania kuzuia na/au kusitisha maandamano ya amani. Badala yake, sheria ziweke wazi wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania kulinda maandamano ya amani na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na/au ya wananchi;
  7. Tume huru ya uchunguzi ya kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) itakayoundwa na majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iundwe ili kufanya uchunguzi huru, wa kina na wa wazi wa matukio yote yaliyopelekea Inspekta Jenerali wa Polisi na/au Jeshi la Polisi la Tanzania kupiga marufuku maandamano ya amani na mkutano wa hadhara na baadaye Jeshi la Polisi la Tanzania kufanya vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia. Tunapenda kusisitiza kuundwa kwa tume huru ya kimahakama kwa sababu historia ya tume nyingine ambazo zimeundwa kwa utaratibu wa Rais kuteua watu anaowataka inaonyesha kwamba zimefanya kazi zao za uchunguzi mafichoni bila kushirikisha wadau wengine na bila wananchi kufahamu kitu kinachoendelea. Matokeo ya tume nyingi za namna hiyo ni kwamba ripoti zake mara nyingi zimepuuzwa na/au kufichwa na watawala. Tume ya uchunguzi ya kimahakama hufanya kazi zake kwa uwazi na huruhusu wananchi kuhudhuria na/au kushiriki moja kwa moja katika kazi za tume kama mashahidi na/au kwa kuhoji mashahidi wengine wanaotoa taarifa kwenye tume hiyo;
Katika kuhakikisha kwamba madai yetu yanatekelezwa, CHADEMA inaelekeza viongozi, wanachama na wafuasi wetu mikoani na Wilayani kuandaa maandamano ya amani nchi nzima ili kulaani mauaji ya wananchi wa Arusha na kudai utekelezaji wa madai haya. CHADEMA Makao Makuu itatuma maafisa wa ngazi za juu wa chama, wakiwemo Wabunge na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kushiriki katika maandamano hayo kwa ngazi za mikoa na wilaya ili kuyaongezea nguvu na hamasa.

MAUAJI YA ARUSHA NA UMUHIMU WA KATIBA MPYA
Mauaji ya wananchi wa Arusha yanadhihirisha wazi umuhimu wa kuwa na Katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu. Hii ni kwa sababu, Katiba viraka inayotumika sasa hivi haiheshimiwi hasa na watawala wenyewe kama tulivyoonyesha kuhusiana na uhuru wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara. Aidha, Katiba yetu na sheria nyingine kama vile Sheria ya Jeshi la Polisi na ya Vyama vya Siasa zimetoa mamlaka makubwa mno kwa watendaji kama vile mapolisi kuingilia na kuvuruga haki za wananchi. Mamlaka haya ya kisheria hayana udhibiti wowote wa maana ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania linajiona kama liko juu ya sheria na haliwajibiki kwa makosa yoyote yanayofanywa na Jeshi hilo dhidi ya wananchi.
Aidha, matukio yaliyopelekea Mauaji ya Arusha yanaonyesha kwamba mfumo mzima wa kisheria na kitaasisi wa kuendesha chaguzi katika nchi yetu unahitaji mabadiliko makubwa. Matokeo ya uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini – kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine walikoshinda wagombea wa upinzani - yalitolewa baada ya shinikizo kubwa la nguvu ya umma na sio kwa sababu ya utashi na/au uadilifu wa wasimamizi wa uchaguzi. Na kilichotuleta hapa leo ni matokeo ya uchakachuaji wa uchaguzi wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na viongozi wengine wa Halmashauri hiyo.
Sasa ni muda muafaka wa kuhakikisha kwamba tunapata Katiba mpya itakayohakikisha kwamba vyombo vya ulinzi wa wananchi vinakuwa chini ya udhibiti halisi wa wananchi na/au vyombo vyao vya uwakilishi. Sasa ni muda muafaka kuhakikisha kwamba tunapata Katiba mpya itakayohakikisha kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni huru na wa haki kwa watu na vyama vyote. Sasa ni muda muafaka kuhakikisha tunakuwa na Katiba mpya itakayohakikisha kwamba siku za huzuni kama ya leo zinabaki katika kumbu kumbu za kihistoria tu. Na kwenye suala hili la Katiba mpya tunaujulisha umma wa Watanzania kwamba hatukubaliani hata kidogo na utaratibu uliopendekezwa na Rais Kikwete wa kuunda Tume ya Kupitia Katiba. Utaratibu uliopendekezwa ni ule ule uliotufikisha hapa tulipo. Ni utaratibu wa kubadili Katiba wa watu wale wale unaoendeshwa na/au kusimamiwa na watu wale wale kwa manufaa ya watu wale wale.
Utaratibu ambao CHADEMA itauunga mkono na kushiriki kikamilifu ni ule utakaowezesha kufanyika kwa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba ambao utawakilisha makundi yote ya kijamii katika uundaji wa Katiba mpya. Utaratibu wa kusubiri fadhila za Kikwete za kuteua wajumbe wa Tume ya Katiba haukubaliki tena na CHADEMA haitaubariki kwa kushiriki. Aidha, CHADEMA itatumia uwezo wake wote kuhamasisha wananchi nchi nzima ili kupinga utaratibu unaopendekezwa na Kikwete na kuunga mkono utaratibu wa kidemokrasia wa kupata Katiba mpya kwa kupitia Mkutano wa Kitaifa wa Katiba.

  Tamko limetolewa wakati wa heshima za mwisho za marehemu katikt uwanja wa NMC Arusha na mwenyekiti wa chadema taifa Mh. Freeman Mboye (mb) tarehe 12january 2011.
               Source;http://www.chadema.or.tz