Filamu ni njia mojawapo ya kuburudisha na kuielimisha jamii. Utengenezaji wa filamu katika dunia ya leo unawategemea watu wengi sana, lakini jambo la ajabu na ambalo limekuwa likinitatiza siku nyingi ni kwamba, je ni watu wapi hasa muhimu au ili filamu iweze kukamilika inawahitaji watu wangapi? Bila shaka Mtu wa kwanza kukumbukwa ni Mtayarishaji “Producer”, Mwongozaji “Director”, waigizaji “Actors and actresses”.
Ni nadra sana hasa hapa kwetu watu kumkumbuka mwandishi wa mswada“Script writer” hata waandaaji wa tuzo wamekuwa hawawakumbuki kabisa waandishi watu hawa, utasikia tuzo ya Msanii bora wa kike/ Msanii bora wa kiume, Mwongozaji bora, na wala husikii ikizungumziwa tuzo ya Mwandishi bora wa filamu. Je huo ubora wa waigizaji ama ubora wa waongozaji unatoka wapi au na kazi iliyoandikwa na nani?Read more;nuswe.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment