To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Monday, 7 March 2011

Mchungaji mstaafu bwana Ambilikile Mwasapile ajaza watu loliondo kufuata matibabu!!

Pichani mchungaji akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia dawa hiyo na aina za magonjwa yanyotibiwa.
Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni kusubiri kupewa dawa
Sehemu ya foleni kuelekea kijijini Samunge kata ya sale wilayani Ngorongoro.
Huu ndiyo mti unaodaiwa kuwa ni chanzo cha dawa hiyo.
Habari kutoka katika jiji la Arusha zinasema kuwa kuna mchungaji mstafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT bwana Ambilikile Mwasapile amekuwa akitoa dawa iliyo na uwezo wa kutibu magonjwa sugu yakiwemo ya Ukimwi,kisukari na mengine mengi huku akicharge shilingi mia tano kwa kikombe na mashrti yake ni nafuu kwani mgonjwa anatakiwa kutumia kikombe kimoja tu ili kupona ugonjwa unaomsumbua.
Kutokana na khari hiyo mchungaji huyo amejipatia umaarufu na hivyo kuvuta watu wengi ndani na nje ya nchi jirani kama Uganda na Kenya,hivyo kufanya idadi ya watu kuongezeka siku hadi siku na kusababisha msongamano mkubwa wa magari na watu kuelekea kijijini aliko mchungaji huyo.Pia inasemekana baadhi ya watu hao wamekuwa ni wagonjwa ambao wamekuwa wakihitaji matibabu ya haraka japo kutokana na msongamano huo hawajapata tiba na hivyo kufanya hali za afya zao kuendelea kuzolota hata wengine kupoteza maisha wakiwa njiani kuelekea kupata dawa hiyo.
Akihijiwa na vyombo mbalimbali vya habari mchungaji huyo amesema dawa hiyo ni matokeo ya ndoto aliyooteshwa miaka takribani ishirini iliyopita na hivyo kuamua kuifanyia kazi,na aliendelea kusema kuwa chanzo cha dawa hiyo ni mti wa mugarika ambao huchemshwa na maji yake ndiyo huwa ni dawa.
Hata hivyo hali ya watu katika eneo hilo imekuwa si nzuri hasa ukizingatia kuwa hakuna huduma muhimu za kukidhi haja za umati wa watu waliopo na hivyo kuwa na hofu kuwa huenda yakatokea magonjwa mabalimbali ya mlipuko iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kusaidia kuepusha hali hiyo.
picha kwa hisani ya;kilinyepesiblog&mjengwablog

No comments: