Siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa umoja vijana (UVCCM) mkoani Pwani kutoa kauli kali ya kuwataka wajumbe wa sekretarieti ya chama cha mampinduzi waachie ngazi kwa kile alichokiita kushindwa kutimiza wajibu wao wa 'kumsaidia' mwenyekiti wao Rais Jakaya Kikwete.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Maponduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.
Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoani humo, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani Pwani, Bw. Abdallah Ulega.......alisisitiza kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwa ndiyo imekuwa ikitoa siri kwa chama cha upinzani cha CHADEMA.
Secreterieti hiyo inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Akizungumza jana Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.
"Ni haki yao kutoa maoni, sioni cha ajabu hapo, vijana wana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa.
"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Chiligati.
No comments:
Post a Comment