pichani baadhi ya makundi ya waandamanaji wenye hasira.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeazimia kuongeza idadi ya wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Ivory cost kutoka idadi ya sasa ya 8000 hadi kufikia 10000 ikiwa ni ongezeko la wanajeshi zaidi ya 2000.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutokea kwa machafuko zaidi magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha vifo zaidi.
Siku ya alhamiss majeshi ya serikali yamewaua wanawake sita walikokuwa katika maandamano ya kumpinga rais Ghabo ambaye amekuwa akikataa kuachia madaraka baada ya kushindwa kwa uchaguzi miezi mitatu iliyopita,hali ambayo imepelekea vurugu kati ya majeshi yanayomtii rais Ghabo na wananchi.
Hadi sasa imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 365 wamekufa tangu machafuko hayo kuanza mwezi novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment