Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akiongea na wananchi wa liouhudhuria katika ofisi ya hicho mara baada ya mahakama kutengua ubunge wa Godbless Lema jijini Arusha leo.
(PICHA ZOTE NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA)
Mwenyekiti wa chadema Freman Mbowe katikati akitoa hotuba yake kwa wananchi kushoto ni mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nasari na kulia ni Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini mara baada ya hukumu kutolewa.
NA GLADNESS MUSHI,ARUSHA
KATIKA Hali isiyokuwa ya kawaida MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Bw
Goodbless Lema ametenguliwa na mahakama kuu kanda ya Arusha katika
matokeo yake ya ubunge na kisha mahakama hiyo kutangaza hadharani
siyo mbunge
Akisomewa hukumu hiyo mapema leo na jaji mfawidhi kutoka katika kanda
ya sumbawanga Jaji Gabriel Rwakabirira alisema kuwa ameridhika na
ushahidi wa pande zote mbili na ndio maana ametoa hukumu
Jaji Gabriel alisema kuwa alipokea dondoo 10 kutoka kwa wafuasi wa CCM
ambapo alifanikiwa kukubali dondoo 8 na kisha kukutaa dondoo nyingine
mbili kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama.
Alisema kuwa Mbunge Lema alitenda makosa hayo kati ya mikutano 60
ambayo aliifanya katika enzi za kampeni za mwaka 2010 ambapo
alimchafua Mgombea Mwenza ambaye ni Dkt Batilda Burian kinyume cha
sheria
Jaji huyo alifafanua kuwa mbunge huyo alikutwa na makosa nane hali
ambayo inamfanya mpaka sasa angatuke kwenye ubunge kwa mujibu wa
sheria na taratibu za mahakama.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa anamuagiza msajili wa mahakama kwa
kanda ya Arusha kuhakikisha kuwa anapeleka taarifa kwa tume ya
uchaguzi juu ya kuenguliwa kwa Mbunge huyo lakini bado yuko huru
kukata rufaa hata kwa ngazi za juu sana.
Awali Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Arusha Mjini Goodbless
Lema,aliwaambia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika katika viwanja
vya mahakama hiyo kuwa bado yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa
hali hiyo atashinda tu
Lema alisema kuwa kitu kilichofanyika katika mahakama hiyo na kisha
kutengua ubunge wake kiinaonesha wazi jinsi mahakama isivyoweza
kutumia demokrasia na hali hiyo kama itaendelea ni wazi kuwa maskini
watakosa haki zake za msingi
Lema aliwaambia wannachi wa jimbo lake kuhakikisha kuwa kamwe
hawavishiwi roho za uoga kwa kuwa roho hizo za uoga kama zitakuwepo
ndani ya jimbo lake ni wazi kuwa wataendelea kuteseka na CCM
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman
Aikael Mbowe aliwaambia wanachi Jumamosi ndio watajua mbivu na chachu
kama watarudia uchaguzi au watakata rufaa
Kutokana na hali hiyo Bw Mbowe alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa
watulivu kwa kuwa hata chama hicho bado hakina nguvu ya kupingana na
nguvu ya mahakama kwa kuwa mahakama ni muhimili pekee wa nguvu ya
Dola.
No comments:
Post a Comment