To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com
Showing posts with label social. Show all posts
Showing posts with label social. Show all posts

Sunday, 1 May 2011

Ferooz ft Proffesor Jay - Starehe

                        


Tafakari yetu ya leo;
Starehe huwa ni nzuri daima lakini matokeo yake huwa ni mabaya na ya majuto sana,hivyo basi natustarehe lakini tukumbuke sana kuwa wangalifu na matokeo yake.Jali afya yako, maisha yako na familia yako.Walio chini ya umri kuweni na subira,waliokwenye ndoa heshimuni ndoa zenu na mlio single pia tunzeni utu wenu.Na hili ndilo neno la leo.



Wednesday, 13 April 2011

HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAKATI WA MISA YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 27 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA KUU LA MT. PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA TAREHE 12 APRILI 2011 
waziri mkuu mh.Mizengo Pinda.
Siku kama ya leo, tunapokutana kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha Mpendwa wetu, Mzee Edward Moringe Sokoine inakuwa vigumu sana kupata maneno mazuri ya kusema. Inakuwa vigumu kwa sababu ukweli hatuko naye tena, lakini kwa njia moja ama nyingine tunaamsha hisia zetu na upendo wetu tuliokuwa nao kwake na ambaye sasa ametutangulia mbele ya haki.
Faraja ninayoipata Mimi kama Pinda, kwa siku ya leo tunapoadhimisha kumbukumbu kama hii ni kuwa bado huyu mwenzetu tuko naye kimawazo, kiakili na kubwa zaidi kiroho.
Vilevile, kwa mawazo yangu, na kwa kuamini kwangu, siku ya leo ni muhimu kwa kuwa inatukumbusha kuwa sote hapa duniani ni wapita njia na siku moja tutaungana na waliotutangulia mbele ya haki huko Mbinguni.
Leo tunatimiza miaka27 tangu Marehemu Edward Moringe Sokoine atutoke gafla kwa ajili ya gari. Mtakumbuka kwamba Marehemu Sokoine alikuwa Waziri Mkuu kwa vipindi viwili tofauti. Alikuwa Waziri Mkuu wa Tatu wa Tanzania baada ya Marehemu Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere na Marehemu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa.
Alianza kuwa Waziri Mkuu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980. Baadae tena aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu kwa kipindi cha pili tarehe 23 Februari 1983 hadi 12 Aprili 1984 alipofariki kwa ajali ya gari pale Wami Dakawa, Morogoro.
Ninaamini aliteuliwa kwa vipindi viwili tofauti kutokana na imani kubwa aliyokuwa nayo Mheshimiwa Rais kwake. Imani hiyo inatokana na ukweli kuwa alikuwa mchapakazi kweli kweli, mwaminifu, mtetezi wa wanyonge na msimamizi wa kweli wa maendeleo ya Taifa hili.
Tunapomkumbuka siku ya leo, ni dhahiri tunakumbuka Mtu aliyejitolea kwa hali na mali kupambana na Ujinga, Maradhi na Umaskini. Alipigana kufa na kupona kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo.
Tunamkumbuka sana Mzee Sokoine kwa uchapaji kazi wake na utetezi wa Wanyonge.  Atakumbukwa milele kwa jinsi alivyokuwa tayari kutetea maslahi ya wanyonge na kusimamia ujenzi wa Uchumi wa Tanzania.
Atakumbukwa siku zote kwa juhudi zake za kujenga Jamii ambayo inachukia rushwa, Jamii inayochukia Wahujumu Uchumi na Jamii inayochukia Walanguzi. Alipambana na Watu ambao walikuwa wanahodhi bidhaa zisiwafikie Watu wa chini kwa bei halali. Ninakumbuka maneno yake aliyoyasema kwamba “Kama Serikali ilikuwa likizo sasa likizo imekwisha”. Kwa maana hiyo aliwabana Walanguzi na Wahujumu Uchumi na hatimaye wakasalimu amri. 
Marehemu Sokoine alikuwa muasisi wa Biashara huria Nchini wakati tukiwa kwenye itikadi ya ujamaa.  Aidha, alikuwa na wazo zuri la kuanzisha usafiri wa Daladala Dar es Salaam.  Wakati wake Mabasi makubwa ya Ofisini yalitumika kubeba Watu Jijini Dar es Salaam;
Kutokana na juhudi zake, ndiyo sababu kumbukumbu zake ziko katika maeneo mengi Nchini.  Moja ya kumbukumbu hizo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichokoMorogorokwa jina laSokoine University of Agriculture.  Marehemu Sokoine alikuwa mpenzi mkubwa wa Kilimo.  Alipenda Kilimo cha Plau na Matrekta ili kuondokana na Kilimo cha Jembe la Mkono.
Marehemu Sokoine alishiriki kuanzisha dhana ya Nguvu Kazi ili kumfanya kila Mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi kufanya hivyo.  Nakumbuka alitoa mshahara wake asilimia 50 kutunisha Mfuko wa Rais wa Nguvu Kazi.  Mfuko ambao ulisaidia Watu wa kipato cha chini;
Marehemu Sokoine alikuwa Kiongozi wa kipekee.  Tunamkumbuka kwa kile alichoamini kwamba “Uongozi ni Dhamana”. Kwa maoni yake aliamini kwamba, kuwajibika kama Kiongozi ni kukubali kwa hiari dhamana ya Uongozi unayopewa ama kwa njia ya kuomba kwa kura au kwa kuteuliwa Kikatiba au Kisheria. Aliamini kuwa Kiongozi lazima akubali kutumia dhamana ya uongozi aliopewa kwa maslahi ya umma na kwa Taifa kwa ujumla;
 
Kwa misingi hiyo, Marehemu Sokoine alikuwa mstari wa mbele kukubali Kanuni za Chama chake.  Aliamini kwamba Kiongozi hatatumia dhamana ya madaraka yake kujinufaisha mwenyewe binafsi au Mtu mwingine yoyote, bali Taifa zima;
Marehemu Sokoine aliamini kuwa Kiongozi daima atakuwa ni mtiifu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na atamshauri kwa hekima na kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa;
Marehemu Sokoine, pamoja na kupenda kusimamia maendeleo ya Nchi yetu, pia alikuwa Mcha Mungu-Mtu wa Kiroho, mwenye kupenda Dini.  Mtu mwenye kupenda Watu.  Mtu wa Imani. Wote sisi ni mashahidi kwamba Marehemu Sokoine alikuwa Mtu wa Mungu na ili kudhihirisha hili siku aliyopata ajali alipita na kusali katika Kanisa hili kabla ya kuanza kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam. Hiyo ilikuwa ibada yake ya mwisho akiwa hai kabla ya kufikwa na mauti.
Marehemu Sokoine atakumbukwa kwa mengi ambayo kwa kweli tukiyaongelea hapa hatutayamaliza;
 
Ninachoweza kusema, leo tunamkumbuka Mtu ambaye kwetu sisi Watanzania, ni kielelezo bora cha utumishi wa watu, kielelezo cha kujituma, kielelezo cha upendo, kielelelzo cha kupenda haki kielelezo cha kupigania wanyonge na kielelezo cha kumcha na kumtumikia Mungu
Marehemu Sokoine amefanya mengi mazuri ambayo tunayakumbuka leo. Hebu tujifunze kutoka kwake kwambaThe good we do today becomes the happiness of tomorrow” ikimaanishwa kwamba -Mazuri tunayoyafanya leo, huwa furaha ya kesho. Tumuige kwa kufanya mazuri ambayo yatakumbukwa daima na vizazi vijavyo.
Viongozi mliojumuika nasi hapa leo na
Ndugu Waumini;
Nimalizie kwa kuungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Marehemu Mzee Edward Moringe Sokoine kuendelea kumwombea kwa Mwenyezi Mungu ili ampumzishe mahali Pema Mbinguni. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.   AMINA
imetolewa na ofisi ya waziri mkuu.

MDAU NA TAFAKARI YAKE YA LEO!!! JE YULE UMPENDAYE NDIYE?

Moyo wa mtu ni kichaka na watamanianao huonekana wengi bali wapendanao ni wachache na hawajulikani. Hebu fikiria leo Mungu akisema kila moja asimame na ampendaye Je? Wewe utasimama na nani? Na huyu umdhaniaye ukimkuta amesimama na ampendaye utafanyaje? Haaaaaa…..!! Unacheka?Kwa habari hii na nyingine nyingi mtembelee kwenye libeneke lake la maisha na mafanikio kwa;kubonya hapa

Tuesday, 12 April 2011

CCM WASHANGILIA MAKAMBA KUVULIWA UKATIBU!!

WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.Soma zaidi ;kandamiza hapa

WAZIRI MKUU WA ZAMANI E.SOKOINE AKUMBUKWA LEO!!

 Hayati Edward Moringe Sokoine 1938-1984
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Tanzania, marehemu Edward Sokoine, atakumbukwa Jumanne hii kwa ibada maalumu ya kumwombea kuadhimisha miaka 27 tangu kufariki kwake, Aprili 12, 1984.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, katika siku hii, kumeandaliwa ibada maalumu ya kumwombea Hayati Sokoine katika kanisa alilosali mara ya mwisho kabla ya kifo chake mjini Dodoma.Soma zaidi;bofya hapa

CCM YARIA NA MAFISADI NDANI YA CHAMA,YAWAPA MIEZI MITATU KUJIUZURU!!

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa miezi mitatu kwa wanachama wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi wajiuzulu, wakikaidi watawajibishwa.

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, amesema, wanaCCM hao wakiwemo vigogo wanapoteza haiba ya CCM katika macho ya Watanzania.

Kwa muda mrefu, wanachama kadhaa wa CCM wamekuwa wakitajwa kuhusika katika vitendo vya rushwa na wakahusishwa kwenye kashfa kadhaa ikiwemo ya uzalishaji wa umeme wa dharura ya kampuni hewa ya Richmond, kashfa ya Dowans, kashfa ya ununuzi wa rada, na kashfa ya ulipaji wa madeni ya nje kupitia akaunti ya EPA Benki kuu Tanzania (BOT) kupitia kampuni ya Kagoda.

Kwa mujibu wa Kikwete, Halmashauri Kuu ya CCM imezungumza na watuhumiwa hao wakati wa mkutano uliomalizika jana usiku mjini Dodoma, na wameelewana.

“Tusionekane kuwa ni chama ambacho vitendo vya rushwa hatuchukizwi navyo” amesema Kikwete wakati anafunga mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ulioanza juzi asubuhi.

Amesema, CCM imeanza kuchukua hatua, wanaotajwa kuhusika kwenye ufisadi na rushwa wanafahamika, hivyo wasionewe haya, wao wenyewe wawajibike, wasipofanya hivyo ‘wataoneshwa ulipo mlango’.

Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema, chama hicho kimeamua kuwashughulikia WanaCCM wala rushwa na mafisadi.

“Haogopwi mtu, na Mwenyekiti alisema, tumekusudia, tunakwenda kujivua gamba” alisema Nnauye jana usiku wakati anazungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Halmashauri Kuu kwenye jengo la White House mjini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, John Chiligati amesema, watuhumiwa hao wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wanatajwa vibaya kwenye jamii, hivyo wawajibike hata kama hakuna ushahidi.

“Tumewaambia wao wenyewe wapime, wachukue hatua za kuwajibika” amesema na kubainisha kuwa wasipotekeleza waliyokubaliana, CCM itawawajibisha hivyo wasisubiri kuoneshwa ulipo mlango.

Chiligati amewaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, kuanzia sasa, CCM ipo makini kupambana na vitendo vinavyoleta sura mbaya katika chama hicho na amewaambia watuhumiwa kuwa “ usiulize ushahidi upo wapi”

Kikwete ameishukuru iliyokuwa Kamati Kuu ya CCM kwa kukubali kujiuzulu kwa maslahi ya chama hicho kwa kuwa wameonesha wanajali maslahi ya wanachama.

Ameishukuru Kamati Kuu mpya yenye wazee na vijana wasiozidi umri wa miaka 35, na ameishukuru pia iliyokuwa Sekretarieti ya CCM iliyojiuzulu kwa ujasiri wao na kujali maslahi ya chama chao.

Kikwete amesema, anaamini kwamba, Kamati Kuu mpya itakidhi matarajio ya kuijenga upya CCM, na amesema, kuwa miongoni mwa wajumbe ni wakongwe, wawe kama panga la zamani, makali yale yale.

“Tumekubaliana, mwenzetu anayelegalega tunamwambia, mwenzetu unalegalega” amesema Kikwete akimaanisha kuwa, kuanzia sasa hakuna kuoneana haya CCM.
Toka gazeti la Habari leo

SURA MPYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM



SEKRETARIETI KUU, Katibu mkuu Wilson Mkama, Mweka Hazina  CCM taifa Mwigulu Lameck Nchemba,Katibu Itikadi Mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Mnauye,Katibu Organaizesheni NEC Bi Asha Abdullah Juma,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar vuai Ali Vuai na January Makamba uhusiano Kimataifa              
WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU

Anna Abdalah

Peter Kisumo

Mwigulu Nchemba

Januari Makamba

Aly Juma Shamhuna

Wilson Mukama

Emmanuel Nchimbi.

WANAOINGIA KAMATI KUU

Pindi Chana

Abdulrahman Kinana

Zakhia Hamdan Meghji

Abdalah Kigoda

Steven Wasira

Costansia Buhiye

William Lukuvi

Dk. Hussein Ali Mwinyi

Dk. Maua Daftari

Samia Suluhu

Shanmsi Vuai Nahodha

Omary Yusuf Mzee

Prof. Makame Mbarawa

Mohamed Seif Khatibu       

KUTOKA MJENGWA BLOG

Tuesday, 29 March 2011

Waziri wa afya wa Kenya aja na mpya!!Ataka huduma ya Babu Loliondo isitishwe na yeye akamatwe....

Hebu angalia video hii umsikie huyu waziri wa afya nchini Kenya na maoni yake juu ya huduma ya babu kule Loliondo kisha toa maoni yako wewe unalionaje hili je yupo sahihi kuwa huduma hii ifungwe?
Na je hoja ya waziri huyu wa Kenya ni ipi watu kupita njia za panya kuja kwa babu au ni tiba inayotolewa na babu?
Toa maoni yako baada ya kuingalia video hii.

Big shame!!Pastor, wife in showdown in church


There was drama in a church in Kesses, Uasin Gishu County last Sunday when a pastor and his wife quarrelled in church.
The incident, which almost disrupted the Sunday service started when the pastor’s wife stood to welcome the women’s choir. The pastor stopped her when she begun introducing herself and explaining the songs they planned to sing. He explained there was no time left and hence the choir could not sing.
He instructed the congregation to bow down for a prayer. The embarrassed woman objected her husband and instead started singing. She requested the congregation to join her insisting there was enough time to praise God.
The congregation got confused and they did not know whom to follow. The wife, who had introduced herself as Jane, continued to sing while the pastor started to pray. The pastor become angry and took away the microphone from her.
In a fit of bitterness, Jane started shouting to her husband. She accused him of being a pretender leading the Lords sheep astray. She claimed the pastor was unfaithful and she had previously caught him with other people wives.
"I have tolerated you for a long time and at the end you reward me by embarrassing me before the congregation. You are a hypocrite," she said.
The puzzled flock could not believe what they heard and they started to walk out one by one. They gathered in to small groups outside the church to discuss the issue. Some supported the pastor while others sided with Jane.
Meanwhile, Jane announced using the loud speakers that she wanted to divorce her husband. The announcement stirred the congregation and those who were out streamed back into the church to witness the happenings. By the time they got in, the pastor was begging for forgiveness from his wife. Jane was bitter and she went further to accuse her husband of misusing the church funds by purchasing personal property.
The situation was calmed by the elders who could no longer tolerate them washing dirty linen in public. The two were ushered out of the church and they were told to solve their marital issues at home. They were accompanied by some church elders. The congregation was urged to calm down and allow the service to proceed. They refused and demanded the pastor be brought back to explain himself.
A woman stood up and informed the congregation that much of what was said was true. She informed them the pastor was visiting her frequently but after realising what he wanted she stopped him. Two other women confessed the same. The irate congregation threatened to attack the pastor but the elders calmed them down.
The elders left the assistant pastor addressing the flock while they went in the vestry to discuss the issue. After about 20 minutes they came back and the eager congregation was silent to hear their decision.
After apologizing on behalf of the leadership for allowing such a thing to take place in their church, the senior elder stated they would not allow few people to spoil the image of the church. He concluded the elders have decided to excommunicate the pastor from the church until further notice. The followers were happy because of the decision and some said the same should be done to errant members.
Despite pleas from her husband and people who helped them tie a year ago, Jane vowed to divorce the pastor.
"I would rather remain single instead of being a wife to a pretender," she said.
Source;The standard in Nairobi Kenya