Ni hayati mwalimu Julius K. Nyerere na hayati A.A. Karume waasisi wa muungano
Udongo wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar ukichanganywa na kuunda Tanzania moja.
Makubaliano na mkataba ukisainiwa baina ya viongozi wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar wakati wa tukio zima la muungano.
Ndugu wana blog sina hofu kuwa mnakumbuka moja siku muhimu na kihistoria ktk historia ya nchi yetu ambayo huazimishwa kila tarehe 26/04.Siku hii ni ile ambayo waasisi wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar kuamua kuunganisha nchi hizi na kuunda nchi moja ambayo ni Tanzania,
Kulikuwa na sababu lukuki ambazo waasisi hawa walizitumia ktk kuunganisha nchi hizi ikiwa na pamoja na Kibiashara,ulinzi,kijamii na pia kisiasa.lakini sasa hivi ikiwa siku ya leo muungano huu utatimiza miaka takribani 47 kumekuwa na malalamiko mengi toka pande zote mbili kuwa hakuna usawa katika maswala mbalimbali yahusuyo muungano na pia kumekuwa minongono kuwa muungano huu hauna faida na hivyo ni bora uvunjwe.Sasa ndugu wana blog naomba tujadili swala hili kama watu wenye upeo huku tukiangalia faida na pia mapungufu yake.
1.je kuna haja ya muungano kuendelea kuwepo?
2.Na kama haja ipo je tunafikiri nini kifanyike ili kurekebisha hitilafu zilizopo ktk muungano huo?

3. Je unadhani ni kweli kwamba hakuna usawa katika maswala yahusuyo muungano?
Naomba kuwakilisha......toa maoni yako juu ya hili kwani hayo hapo juu ni mawazo yangu tu...
2 comments:
Mimi nina swali la kizushi je kama Tanganyika na Zanzibar tuliungana na kuwa Tanzania kwanini Zanzibar wana rais wao na Tanzania Tuna rais wetu na pia bendera tofauti?
Hapo chacha Yasinta..
Post a Comment