Emmanuel Mutai
Wakenya hapo jana wameonyesha umahiri wao katika mashindano ya mbio yaliyofanyika hapa jijini London nchini uingereza kwa kufanikiwa kushika nafasi zote tatu za juu. Emmanuel Mutai ndiye aliyekuwa kinara kwa kufanikiwa kukimbia kwa masaa mawili, dakika nne na sekunde arobaini 2:04:40 .Mutai alivunja rekodi ya mkenya mwenziye bwana Sammy Wanjiru ambaye hakuweza kuwepo hiyo jana kwasababu ya kuwa majeruhi.
Hata hivyo pia mkenya mwingine alishika nafasi ya pili na huku mwingine akiambulia ya tatu. Ushindi huo wa jana unaashiria kuwepo kwa ushindani mkubwa sana katika mahindano ya Olympic ambayo yanatarajiwa kufanyika hapa nchini mapema mwakani.
No comments:
Post a Comment