Hebu siku ya leo tujikumbushe Asili zetu kila mmoja anapoiangalia video hii na avute hisia za ngoma ya kwao.Hao ni wanyakyusa wakicheza ngoma maarufu Mkoani Mbeya inayojulikana kama Ligoma. Kuna faida mbalimbali ambazo zinatokana na kuchezwa kwa ngoma hizi kwa mfano ushirikiano,upendo na pia burudani kwa jamii husika.Haya wadau kazi kwenu burudani hiyo na wewe kama unayo ya kwenu na unataka iwekwe hapa kibarazani basi usisite kunitumia kwa email hii; maishablog@yahoo.com
2 comments:
Kaka hebu tafuta na Bugobogobo ya wasukuma uone ufundi wa kucheza na majembe..
Nami naisubiri kwa hamu hiyo nione huo ufundi wa Kisukuma!!!
Post a Comment