To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Thursday 13 October 2011

MABADILIKO KWENYE WAVUTI YA WANAVYUO...




Habari za leo wadau wetu na poleni na kazi,Tulikuwa tunaomba msaada wenu. Tunatanguliza Shukrani zetu
Taarifa ya Mabadiliko ya Mtandao wa Matukio na wanavyuo 
Sasa Blog hii imeungana na wanavyuo watanzania wanaosoma nje ya Tanzania
Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.
Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa  taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo(www.tzwanavyuo.blogspot.com) sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania, Tumefanya hivi kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya tanzania kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko, Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari zake ama habari zao hapa. Pia kwa watumishi wa vyuo Hapa nchini Tanzania mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo. Mabadiliko mengine tuliyo yafanya kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania,pia tumeweka na mambo mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.Mtandao wa wanafunzi ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani mnakaribishwa kujiungawww.tzuniversitiesconnects.tk mnakaribishwa sana pia mtakutana na wanavyuo wengine.Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati.

Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa: twanavyuo@live.com
Tembelea Mtandao wa Matukio na wanavyuo hapa

Kwa niaba ya wanavyuo wote,
Matukio na wanavyuo Crew.

No comments: