To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Sunday, 23 October 2011

WAHUSIKA TUNAOMBA MLIANGALIE HILI-KAWEpichani bonde la mbezi ambalo pia ni mpaka wa kawe na mbezi likiwa katika hali ya uchafu. 

 Maporomoko yanayotokana na mashimo yalimo chimbwa mchanga
 Sehemu ya mlundikano wa taka katika eneo hilo la bonde
Wananchi wasio waadirifu na kujali mazingira wakiendelea na shughuli za uchimbaji mchanga richa ya kukatazwa na mamlaka husika.

*****Na mwandishi wetu******
Mwandishi wa blog hii ya maisha ameripoti hali tete kutoka katika maeneo ya mpakani mwa mbezi na Kawe inayosababishwa na uchafuzi pia nuharibifua  wa mazingira mkubwa unaofanywa na watu wa maeneo hayo bila kujali afya, usalama lakini pia mazingira kwa ujumla. Katika eneo hili limekuwepo dampo kubwa lisilo rasmi ambapo kila mkaazi wa eneo hili hutupa taka za aina yoyote ile jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi cha mvua za masika.Lakini pia wakazi hao wamekuwa wakichimba mchanga kwenye bonde hilo na hivyo kudsababisha uharibifu mkubwa sana wa mazingira jambo ambalo ni hatari kwa majengo yaliyo karibu na bonde hilo.Pia kuna kundi la vijana katika eneo hili maarufu kama (mateja)kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa nne usiku ambao huchangisha fedha kutoka kwa wananchi kwa madai kuwa wanatengeneza kivuko kwenye bonde hilo na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa wakazi na wapitanjia kwenye eneo hilo. Vijana hao wakati mwingine wamekuwa wakipora vitu vya thamani kama simu za mkononi na fedha na hata ripoti zinapopelekwa kwenye vyomba vya dora hakuna hatua zozote za kudhibiti zinazochukuliwa kupambana nao.
Hivyo basi ni rai yetu kwa viongozi husika kwani wanataarifa hizi na wengine hupita hapo na kujionea yanayotokea kuchukua hatua za makusudi ili kunusuru wananchi pia mazingira ya eneo hili.

No comments: