copyright;maisha blog
baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye maandamano.
Habari kutoka mkoani Iringa zinasema kuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini na wale wa chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa wapo kwenye mgomo ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono wenzao wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam kuishinikiza serikali kuwaongezea posho zao kutoka shilingi 5000 ya sasa hadi shiling 10000.
Mgomo huo umekuja siku chache baada ya waziri mkuu kuahidi kuunda tume itakayopitia madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu madai yao kupanda kwa hali ya maisha na hivyo kupelekea hela wanayopata kwasasa kuwa haiwatosherezi.
Hadi sasa hakuna taarifa zozote za vurugu wala matumizi ya nguvu za dora yaliyo ripotiwa kutokea kwenye maandamano na mgomo huo.
Picha toka:Francis Godwin blog
No comments:
Post a Comment