To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Friday, 26 November 2010

Safari ya sugu toka katika muziki hadi ubunge!!

                                                                 Mh; Joseph Mbilinyi
Jina Sugu ktk fani ya mziki ni moja ya majina makongwe na yaliyopata umaarufu mkubwa nchini Tanzania hasa ktk miondoko ya rap.Sugu amekuwa ktk gem kwa mda mrefu sana na hivyo kuwa na mashabiki wengi ndani na nje ya nchi ya Tanzania, na amekuwa akisifika sana ktk utunzi wa mashairi yakuelimisha jamii,kufundisha,kukosoa na pia kukemea wakati inapobidi.Hiyo kama haitoshi akaamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuwakilisha wananchi wa Mbeya mjini ktk nyumba ya kutunga sheria jambo ambalo binafsi nampongeza sana.Najua huenda watu wengine watakuwa na mashaka juu ya uzoefu wake lakini naomba tusitoe hukumu bila kuona utendaji wake wa kazi bali sote kwa pamoja kama wananchi wa Mbeya mjini wakati umefika sasa kuweka tofauti zetu za kisiasa pembeni na kushirikiana na mbunge wetu huyu kuleta maendeleao ktk mkoa wetu.Naomba nimalize kwa kumtakia kila la kheri mheshimiwa Sugu ktk safari yake mpya ya kisiasa.Mungu ibariki Tanzania na africa wa ujumla.Naomba kuwakilisha.

No comments: