To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Sunday, 12 December 2010

Tanzania mabingwa wapya tusker cup!!!!!!

 Kikosi cha Kilimanjaro stars kilichotwaa ubingwa wa tusker.
Kikosi cha wapinzani timu ya taifa ya Ivory cost.
Leo hii tarehe 12 december kulikuwa na mpambano mkali wa mchezo wa fainali kuwania kombe la tusker ambao ulizikutanisha timu za taifa toka Ivory cost na wenyeji Tanzania, mchezo huo ulikuwa wa vuta ni kuvute na wenye msisimko wa namna yake hasa ukizingatia kuwa uwanja ulijaa mashabiki waliokuwa na kiu ya mda mrefu ya mafanikio ya soka kwa timu yetu ya taifa.Hata hivyo vilio na maombi ya watanzania vilisika pale dakika ya 31 ambapo nahodha wa timu ya kilimanjaro stars Shadraki Nsajigwa  aliipatia bao la kuongoza timu yake kwa mkwaju wa penati ambayo ilitolewa baada ya mmoja wa mabeki wa timu ya Ivory cost kuunawa mpira katika eneo la hatari,goli hilo lilidumu na ndilo lililoleta shangwe kwa Tanzania na kupeleka majonzi kwa wapinzani wetu.Hivyo basi mashindano hayo yamemalizika huku timu ya Ivory cost kutwaa nafasi ya pili na majirani zetu Uganda nafasi ya tatu.
Mungu ibariki Tanzania na Africa kwa ujumla...............

No comments: