To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Thursday, 6 January 2011

News update!Viongozi wa chadema wapandishwa kizimbani...Na serikali yatoa tamko juu ya sakata hilo.


Habari zilizoifikia blog ya maisha hivi punde zinasema kuwa viongozi wa chama cha Chadema akiwepo mwenyekiti mh Freeman Mboye, katibu wake Dr Wilbroad Slaa na wafuasi wengine wapatao 31wamefikishwa mahakamani katika mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomewa mashitaka ya kuandaa maandamano bila ya vibali vya polisi.kati yao wafuasi 6 waliosomewa mashitaka wakiwa hospiatlini ambako wanauguza majeraha waliyoyapata hapo jana wakati wa vurugu kati ya waandamanaji na polisi wa kikosi cha kuzuia ghasia.Habari zaidi pia zinasema serikali imeingilia kati sakata hilo na kuzitaka pande mbili zinazopingana kukaa chini kwa pamoja na kutafuta suluhu ya tatizo lao kwa amani ili kudumisha mshikamno katika jiji la Arusha.Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya ndani mh Shamsi V. Nahodha alipongea na wandishi wa habari jijini Dar hii leo.

1 comment:

Anonymous said...

Wilbrod silaa ametangazwa kuwa anayo bastola
Na bastola na siri ya mtu binafsi je?utakuwaje?