To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Sunday, 20 February 2011

Wadau wahamasishwa kusaidia wahanga wa mabomu Gongolamboto!!

copyright;maisha blog
 Baadhi ya wakazi wa gongolamboto na maeneo ya jirani wakiwa katika uwanja wa uhuru wakiwa na nyuso za huzuni wakisubiri kujua hatima yao
Mh..makamu wa rais Ghalib Bilali akitoa pole kwa baadhi ya  waathirika wa mlipuko wa mabomu katika hospital ya Amana jijini Dar pichani hapo juu.
Naomba kutoa wito kwa wadau mbali mbali nchini na nje ya nchi kuchangia wahanga wa mlipuko wa mabomu huko gongolamboto na maeneo ya jirani ili kuwasaidia kurudia hali yao ya maisha ya kawaida.Wakazi hao ambao wengi wao wamepoteza ndugu na jamaa waliokuwa wakiwategemea,wengine mali zao kuharibiwa vibaya na hata wengine kukosa mahala pa kuishi wamekuwa wakihitaji sana misaada mabalimbali yakijamii ili kuweza kujikimu kimaisha.Hivyo basi shime ndugu watanzania popote pale tulipo na tuweni na moyo wa huruma na kuchangia waathirika hawa kwani kwa namna moja ama nyingine ni ndugu zetu,familia na pia wananchi wenzetu.Kwa kufanya hivyo basi mwenyezi mungu atatuzidishia zaidi na pia tutaokoa maisha ya hao ndugu walio katika wakati huu mgumu.Mwisho naomba kuwapa pole ndugu wote walio patwa na janga hili.

No comments: