To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Thursday, 17 February 2011

Sakata la Mlipuko wa mabomu kambi ya jeshi ya gongolamboto;Waziri wa ulinzi akumbushwa ahadi yake ya kujiuzuru!!!!

copyright;maisha blog


Picha za baadhi ya wahanga wa mlipuko wa mabomu uliyotokea jana usiku maeneo ya gongolamboto.
Sakata la mlipuko wa mabomu uliyotokea hapo jana jijini Da-es-salaam katika maeneo ya kambi ya gongolamboto umechukua sura mpya kwani wanaharakati na asasi mbali mbali zinamtaka mh. waziri wa ulinzi ajiuzuru kutokana na matukio haya ya mlipuko wa mabomu kuwa unajitokeza mara kwa mara na kusababisha maafa makubwa na uharibifu wa mali za wananchi wasio na hatia.
Mwaka jana tumeshuhudia maafa makubwa katika kambi ya jeshi mbagala nakwa maelezo ya wahusika waliahidi hali hii kutojitokeza tena japo imekuwa kinyume chake kwani ndani ya kipindi kifupi hali hiyo imejitokeza tena na kusababisha maafa kama yale ya kipindi cha nyuma.
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mlipuko wa jana unasadikiwa kufikia zaidi ya watu kumi na kuwaacha wengine wakiwa majeruhi na hata wengine kupotezana na familia zao.
picha kwa hisani ya ;michuzi blog

No comments: