To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Tuesday, 12 April 2011

CCM WASHANGILIA MAKAMBA KUVULIWA UKATIBU!!

WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.Soma zaidi ;kandamiza hapa

No comments: