Mabaki ya bus la sumry baada ya ajari
Basi la sumry linalofanya safari zake kati ya Arusha na Mbeya hapo jana limepata ajari mbaya na kusababisha vifo vya watu 13 na kuwaacha wengine wakiwa ni majeruhi na vilema wa viungo. Ajari hiyo ambayo kwa mujibu wa shuhuda wetu imetokea mpakani mwa mkoa wa Iringa na Mbeya usiku wa kuamkia jumamosi. Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni kupasuka kwa tairi za bus hilo na hivyo kumshinda dereva na kupinduka. Kazi ya kutambua maiti na majeruhi bado inaendelea na huku ikitajwa kuwa mmoja wa waliopoteza maisha kuwa ni dereva wa gari hilo bwana Makame Juma na kuwa na shaka huenda hata kondakta akawa amepoteza maisha katika ajali hiyo. Maiti nyingine zimehifadhiwa katika hospitali ya wazazi meta na Rufaa mbeya mjini kungoja kutambuliwa. Taarifa zaidi juu ya tukio hili zitaendelea kutolewa pale
zitakapo patikana na tunapenda kuwapa pole waliopatwa na msiba na pia walionusurika kwenye ajali hiyo.
picha na Mbeya yetu blog
No comments:
Post a Comment