To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Tuesday 17 May 2011

Bingwa wa Olimpiki Kenya Samweli Wanjiru afariki!!

Samweli Wanjiru enzi za uhai wake

BINGWA wa Olympiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya, Samuel Wanjiru ameaga Dunia kwa kile kinachosemekana kwamba amejiua.Duru za polisi
zinasema, Wanjiru alikumbana na mauti hayo baada ya kuruka kutoka chumba chake cha ghorofa moja katika eneo la Nyahururu, Mkoa wa Kati wa Kenya.

Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema kwamba uchunguzi umeanza, ili kubainisha sababu za kifo hicho.

Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za Olimpiki mwaka wa 2008 mjini Beijing, kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:06:32 na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume.

Wanjiru pia alikuwa bingwa wa Dunia katika misururu ya mbio za marathon, maarufu kama World Marathon Majors kuanzia mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010.

Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilometa 21 kwa kuandikisha muda wa dakika 58:33.

Decemba mwaka jana, Wanjiru alifikishwa mahakamani, kwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.

Mapema mwaka huu, Wanjiru alihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani akiwa anatoka Nairobi kwenda Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa mbio za London Marathon.
habari toka gazeti la majira

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole wanafamilia na pole waKenya pia pole Dunia nzima kwa kumpoteza mwanariadha maarufu. Marehemu astarehe kwa amani.

Goodman Manyanya Phiri said...

Nasoma pahala (http://en.wikipedia.org/wiki/Samuel_Wanjiru) na pengine pia eti mama yake marehemu anamshutumu mke kuwa ndie "kamsafirisha". Mama wakwe nao!!!


Lakini tuachie polisi wafanye uchunguzi wao kabla ya kutoa maoni yetu kwa jazba tupu!


Hapo tena marehemu aliwahi kupatikana na bunduki?? Kwani yeye alikuwa pia mwanajeshi? Kwa hiyo amekufa eti kimwanajeshi???!!! (Au mke wake huyo naye alikuwa na ihawala wa kijeshi wakumsaidia kuua mwanajeshi mwenzie?)


Makubwa!