To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Friday, 17 June 2011

CCM YAIBEZA BAJETI YA UPINZANIUTANGULIZI:
Leo tarehe 15/06/2011 kambi ya upinzani bungeni ambayo inaundwa na chama cha CHADEMA kupitia waziri wake kivuli wa fedha Mhe. Zitto Kabwe (Mb), imewasilisha bajeti yake aliyoiita bajeti mbadala kwa mwaka wa fedha 2011/2012.Nichukue nafasi hii kumpongeza kijana mwenzangu kwa uwasilishaji wa bajeti na kwa baadhi ya mambo ya msingi yaliyomo ndani ya bajeti husika.Hata hivyo bajeti imeacha maswali kadhaa bila majibu.Katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa imedhihirisha kuwa maneno mengi na ahadi nyingi zilizotolewa na CHADEMA wakati wa Uchaguzi kama sio zote basi nyingi zilikuwa ahadi hewa zilizolenga kuwa hadaa wapiga kura kwa nia ya kupata kura.

MANTIKI YA HOJA:
Moja kati ya misingi mikuu ya kutengeneza bajeti katika mazingira ya siasa za kwetu na nyingine nyingi duniani ni ahadi ambazo chama kimeahidi kwa Wananchi wake aidha kwa kupitia Ilani ya Uchaguzi au ahadi binafsi za Mgombea Uraisi alizozitoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi. Kwa maneno mengine bajeti ni zao la Ilani ya Uchaguzi ya Chama husika na sera mbalimbali zilizopo.
Soma zaidi hapa

Pia kwa kuisoma bajeti nzima ya upinzani (Chadema) ingia hapa

No comments: