To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Monday, 6 June 2011

MCHUNGAJI AHUKUMIWA KWENDA JERA MIAKA SITA MJINI IRINGA....



Katika kudhihirisha kuwa hizi ni siku za mwisho hapo jana mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Iringa imemhukumu mchungaji wa KKT dayosisi ya Njombe ambaye pia alikuwa ni mwalimu wa shule ya sekondari inayomilikiwa na kanisa hilo ya Pomerini iliyopo mjini Iringa.Mwalimu huyo amehukumiwa kwa makosa mawili likiwemo la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake kosa ambalo adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano au mwaka mmoja jera, na kwa kosa la pili ni kujaribu kumbaka mwanafunzi wake kosa ambalo adhabu yake ni kwenda jera miaka mitano. Adhabu hiyo imetolewa kwa mchungaji huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine popote pale walipo..
Toka Francis Godwin blog

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Na ndio maana taifa la Tanzania litazidi kusifiwa tu kwa ubinadamu wake wakati nchi zingine zinaodai ustarabu zaidi, wenye kuomba rushwa ya ngono pamoja na wanafunzi wao wadhaifu wanazidi kupewa vyeo vya juu! Soma hapa http://goodmanmanyanyaphiri.blogspot.com/2011/04/how-bobelo-zini-prostituted-herself-for.html