To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Sunday, 21 August 2011

UBALOZI WETU UINGEREZA WAFUTARISHA

Afisa ubalozi bwana Zamarani akiwakaribisha wadau kwenye futari ya pamoja
Aziza Ongala (kushoto) ambaye pia ni mtoto wa marehemu Ongala pichani akiwa na Frank
 Dada Carol kutoka ubalozini akiwa amepozi na Jestina kwenye hafla hiyo.
 Fredy MAcha katikati akiwa na wadau wakibadilishana mawazo.
Kwa habari na picha zaidi;kandamiza hapa

************** 
Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa  na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.
Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.
Asanteni Sana,
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIANo comments: