To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Sunday 21 August 2011

BAND YA MSONDO NGOMA YAPATA TUZO (EAST AFRICAN AWARDS)

Na Rajabu Mhabira
BENDI ya mziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group
katika East Africa Music Awards mashindano yariyofanyika Nairobi Kenya
na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo
kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akisibitisha ushindi uho meneja
wa bendi Saidi Kibiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo,
Rajabu Mhamila , Super D
Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa
mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ng'ang'ari
popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D
(pichani)Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na
sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia
kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani
Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja
vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika
Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fulsa ya kupiga nayo
picha katika viwanja hivyo
Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na
Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu

No comments: