To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Saturday, 15 October 2011

NA HILI LA UBUNGO LINASUBIRIA JANGA LITOKEE NDIPO TUME IUNDWE?

 Pichani ni wafanya biashara wadogo(machinga) wakifanya biashara karibu kabisa na mitambo ya kusambaza umeme Ubungo
Picha nyingine ikionyesha msongamano wa wafanyabiashara, waenda kwa miguu na pia magari katika barabara ya mandera.

****Na mwandishi wetu****
Hapo jana maeneo ya ubungo mwandishi wetu amejionea hali isiyo ya usalama katika maeneo hayo ambapo wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wamekuwa wakifanya biashara katika mazingira hatarishi sana hasa ukizingatia kuwa eneo hilo limezungukwa na mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha ya wafanya biashara lakini pia waendao kwa miguu na wanunuzi. Hatari hiyo inatokana na ukweli kwamba watu huwa wengi jioni katika eneo hilo jambo linaweza kusababisha maafa makubwa sana iwapo jamga la moto litatokea ktk eneo hilo.
Daima kinga ni bora kuliko tiba hivyo ni ombi lete serikali kuliangalia jambo ili kwa upana zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia alama za kiusalam ili kuepusha janga lolote kutokea katika eneo hilo badala ya kusubiri janga kutokea ndipo ikumbukwe kuunda tume ya kuchunguza wakati tayari maisha ya watu wasio na hatia yatakuwa yamepotea.

No comments: