To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Wednesday 26 October 2011

OFISI YA TCI YAFUNGULIWA JIJINI MBEYA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini mjini mbeya hivi karibuni
Akizindua ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango, Amesema tumefungua ofisi za kituo hiki katika kanda hii ili kiweze kuwa karibu na wadau wote yaani wafanyabiashara, wakulima, wavuvi na wengine ili kupeleka maendeleo mbele,” alisema Balozi Mtango.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond
Mbilinyi alisema Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini umeiva kiuwekezaji na kuzinduliwa kwa
kituo cha TIC itakuwa ni chachu ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufurika kuwekeza.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkaribisha waziri  Mary Nagu alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Kiwira.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji jijini Mbeya
picha zote na www.mbeyayetu.blogspot.com

No comments: