To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Tuesday 15 November 2011

VURUGU ZA MBEYA: BAADA YA KUPIGWA BOMU LA MACHOZI WAGONJWA WAKIMBIA, MADAKTARI WAWILI NA WAUGUZI WATANO WAZIRAI.

Vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wangonjwa katika Zahanati ya Ipinda, iliyopo Mwanjelwa jijini Mbeya vikiwa wazi baada ya wagonjwa kukimbia mara baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.

Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.
Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akionesha Bomu la machozi lililopigwa na Jeshi la polisi na kuingia ndani ya Wadi.


Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa.

Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya.

Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akiwa ameshika kigae kilichodondoka mara baada ya bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.
PICHA ZOTE NA: www.mbeyayetu.blogspot.com

 

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Sijui mwaka huu vupi huko Mbeya jamani.. Poleni sana wote wajeruhiwa na wengine wote.