To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Wednesday 11 January 2012

NEW ALERT...MZEE KIPARA WA KAOLE AFARIKI DUNIA


[Mzee+Kipara+1.jpg]

Msanii Mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini, Fundi Saidi almaarufu kwa jina la kisanii Mzee Kipara amefariki mapema leo asubuhi,nyumbani kwake huko Kigogo Mbuyuni-Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922,huko Bongoni mkoani Tabora,alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu,alikuwa hawezi kusimama  mwenyewe,sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo,hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda  mwingi kitandani,wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.
Mzeee Kipara alianza sanaa  mnamo mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani na baadaye akachukuliwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa TBC Taifa. Akiwa na kituo hicho, aliigiza katika michezo mingi na nafasi zake kubwa zilikuwa zile zenye kuonesha utemi, wengi huita ukorofi. Mnamo Mwaka 1999, akiwa na wasanii wenzake akina Zena Dilip, Rasia Makuka, marehemu Rajab Hatia  ‘Mzee Pwagu’ na Mama Haambiliki walijiunga katika Kundi la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake katika Runinga ya ITV.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Pole waFamilia, ndugu, marafiki na waTanzania wote kwa msiba huu mkubwa. Mungu alitoa na Mungu anachukua.Pumzika kwa amani.