To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Saturday, 7 April 2012

WATANZANIA WAOMBOLEZA MSIBA WA MSANII KANUMBA NYUMBANI KWAKE VATCAN SINZA..MSANII LULU AHUSISHWA NA KIFO HICHO ASHIKILIWA NA POLISI KWA MAHOJIANO..



Picha za baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa msanii Steven Kanumba huko Sinza .
Pichani ni msanii Elizabeth Michael maarufu kamaLULU  ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji hayo(Bado haijathibitishwa na vyombo husika)

Ndugu wa Kanumba akihojiwa

TAARIFA kutoka kwa ndugu wa Marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa akiishi nae Sinza jijini Dar es Salaam na wakati mauti yanamkuta Kanumba alikuwapo nyumbani hapo zinasema chanzo cha kifo chake ni ugomvi baina ya kanumba na Msanii mwingine wa kike ambaye ni rafiki yake.

Ndugu huyo amepasha kwa wanahabri kuwa Msanii huyo wa kike ambaye analikuwa na mahusinao na marehemu kuwa ni Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu.

Akisimulia kwa ufupi chanzo cha kifo hicho cha Ghafla cha Nguli wa Filamu za Kibongo “ Bongo Movie” anasema wakiwa hapo nyumbani alifika Lulu majira ya usiku.

Anasema aliwaacha wawili hao wakizungumza klakini baade alisikia kuwepo kwa malumbano na wakahamia chumbani ugomvi ukazidi kuendelea. 

Anasema kuwa mara alitoka Lulu na kumita yeye na kumwambia kuwa kanumba ameanguka na alipoingia chumbani humo alikuta kweli ameangua na ndipo alichukua uamuzi wa kumtafuta daktari wake aje kumtibu.

Anasema ndugu huyo kuwa wakati ameruidi ndani humo na Daktari Lulu alikuwa amesha toweka ndipo wakachukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya taifa Muhimbili ambako mwili wa marehemu ulihivaziwa hadi hivi sasa kuendelea na uchunguzi zaidi.

Aidha habari zaidi zinasema kuwa tayari mwana dada huyo maarufu katika ulimwengu wa Filamu za Bongo yupo mikononi mwa Polisi na alikuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Mkoa wa kipolisi cha Kinondoni pale Oystebay Polisi jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni katika kipindi cha Mikasi kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel 5 Lulu mbali na mahojiano mengine aliulizwa juu ya uhusiano wake na msanii huyo na kukataa kata kata kuwa hana mahusiano nae ya kimapenzi isipokuwa ni usanii pekee ndio unawaweka karibu.

Tutaendelea kuwaopasha zaidi juu ya mkasa huu. Lakini niwazi kama kweli Lulu alikuwepo nyumbani hapo na katika purukushani za kutofautiana na Kanumba ndio zimepelekea kifo chake basi atafunguliwa mashitaka na huenda ikawa ni mauaji pasi kukusudia inategemea na uchunguzi utakavyo fanyika. 
Habari kwa Hisani ya Father Kidevu Blog



No comments: