To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Wednesday, 23 February 2011

Gaddafi avunja ukimya Asema....kamwe sijiuzuru hadi tone la mwisho la damu yangu!!!

copyright;maisha blog
Kanali  Gaddafi;rais wa Libya.
Licha ya vurugu na maandamano yanayoendelea hivi sasa huko nchini libya kumtaka kiongozi wa nchi hiyo aliyowaongoza kwa takribani miaka arobaini kanali Kaddafi kuachia ngazi na kuwapa nafasi wengine kushika wadhifa huo ili kuongeza kasi ya maendeleo nchini humo kupamba moto,hapo jana kiongozi huyo ameishangaza dunia pale alipojitokeza hadharani kwa kujiamini na kusema kamwe hatoachia ngazi hadi tone la mwisho la damu yake,aliongeza kusema kuwa yeye hamwogopi mtu yeyote katika dunia hii na anafanya lile ambalo litafaa kwake na kwa walibya.Huku akishangiliwa na badhi ya viongozi wa juu jeshini pamoja na wafuasi wake kiongozi huyo dikiteta alisema ataendeleza mapambano na makundi ya watu wanaompinga na atahakikisha anawadhibiti kisha yeye kubaki huru na kuendelea kuiongoza nchi hiyo ya libya.
Inasemekana pia kiongozi huyo aliyechukua uongozi kwa nguvu miaka arobaini iliyopita anamwandaa mwanae kuwa ndiye atakayemrithi kiti hicho cha urais jambo ambalo pia linapingwa vikali na wananchi wa Libya,japokuwa mtoto huyo wa Gaddafi hadi sasa amekuwa akijishughulisha sana na mambo mabalimbali yanayohusu chama na pia amekuwa akimwakilisha kiongozi huyo katika mikutano mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongea na wandishi wa habari ndani ya nchi.
Imeripotiwa hadi sasa watu zaidi ya 200 wamefariki dunia kwenye maandamno hayo na pia maelfu ya walibya pia wamekuwa wakivuka mpaka kuelekea nchini Misri kuepuka shari zaidi.Na pia makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yamejitokeza kulaani vikali mauaji hayo ikiwa ni pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali  wameungana kupinga hali iyo.

No comments: