LEO ni Mei 21 siku ambayo Taifa linaingia kwenye kumbukumbu chungu ya kutimia miaka 15 tangu kutokea kwa ajali mbaya ya Mv Bukoba iliyochukua maisha ya Watanzania zaidi ya 300 waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza.
Mara kadhaa watu wachache walionusurika katika ajali hiyo wamekuwa wakijitokeza kutoa ushuhuda wao jinsi mambo yalivyokuwa wakati Meli hiyo ilipoinduka ikiwa inakaribia kuingia Bandari ya Mwanza.
Kitu cha ajabu ni kuwa mpaka leo serikali inaonekana bado iko usingizini katika kuweka umakini kwa vyombo vya usafiri nchini jambo linalofanya kuwepo kwa ajali za mara kwa mara zinagharimu maisha ya watanzania wengi kwa uzembe wa watu wachache.
Siku za hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia ajali mbaya za barabarani ambazo zimekuwa zikiacha historia na majonzi kwenye familia mbalimbali,pia kupoteza nguvu kazi ya taifa. Hivyo ni ombi na vilio vya wananchi kwa serikali, waendeshaji vyombo vya usafiri na wadau mabalimbali wa sekta hii kuwa makini katika kudhibiti aajari zisizo za lazima kutokea....
Mwisho naomba kuwapa pole wahanga wa ajari ya MV Bukoba na watanzania wote kwa ujumla mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwafariji.
toka G5
No comments:
Post a Comment