To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Saturday, 17 September 2011

MBOWE ATEMBELEA WALIOUNGULIWA NA SOKO MWANJELWA, AWAPA POLEMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA bwana Freeman Mbowe.

· Uholela wa ujenzi wachangia
· Mikopo yawaliza wananchi
· Rushwa katika ujenzi, Mamlaka yalaumiwa

= = =  = 

Na mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe ametembelea soko liloloungua na Mwanjelwa Mbeya na kuwapa pole wahanga wa moto huo.

Mbowe amesema Serikali inapaswa kuwafidia wafanyabiashara hao kutokana na uzembe uliofanyika ikiwemo kutokuwa na mpangilio mzuri wa soko hilo uliosababisha kikosi cha zima moto kushindwa kuudhibiti moto huo.

Kiongozi huyo wa Chadema baada ya kuwapa pole wahanga hao ameendelea na ziara yake katika kata za Majengo na Nzovwe Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa nafasi ya udiwani katika kata hizo.

Hata hivyo utata wa mfululizo wa matukio ya kuungua kwa masoko yaliyopo mkoani Mbeya kunakosababishwa na moto umeendelea kuligubika Jiji la Mbeya baada ya soko la Sido kuungua mwishoni mwa wiki.
Uchunguzi uliofanywa baada ya soko hilo kuteketea kwa moto umebaini kuwa kikosi cha zima moto kilishindwa kuuzima moto huo kutokana na ujenzi holela uliopo katika soko hilo.
     Uholela wa miundombinu hiyo umetokana na Rushwa kwa watendaji hasa maafisa mipango wa Jiji hilo ambao awali walipima soko hilo na baadaye wafanyabiashara wakaendelea kujenga sehemu za zilizo wazi huku Mamlaka zikiendelea kutoza ushuru kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Aidha baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na chanzo chetu cha habari hii, eneo hilo la tukio walisema kuwa licha ya miundombinu mibovu ambayo haikuwezesha gari la zima kuingia ndani ya soko lakini pia gari za kikosi hicho kimsingi hazina uwezo kutokana na ujazo wake wa maji kuwa mdogo hali iliyokuwa ikipelekea kuishiwa maji haraka.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa suala lingine linalowaliza wafanyabiashara hao mbali na vibanda na maduka yao kuungua ni pamoja na mikopo ya fedha waliyokuwa wamekopa katika idara za fedha yakiwemo mabenki.
       Kwa upande wa Serikali imeshindwa kutoa ufafanuzi wowote juu ya janga hilo ambapo Katibu tawala wa mkoa wa Mbeya Bertha Swai jana jioni aliomba waandishi wa habari kutomuuliza maswali juu ya janga hilo jambo ambalo limeendelea kuwa kizungumkuti kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Moja ya chanzo kinachoelezwa kuwa kilisababisha moto huo ni kwamba ulionekana moshi ukitoka katika moja yakibanda cha chakula kilichokuwepo ndani ya soko hilo, chanzo ambacho kimeipumbaza Serikali na kujikita hapo.

Chanzo hicho kimekuwa sugu midomoni mwa viongozi wa Serikali ambapo Desemba Mosi mwaka 2010 lilipoungua soko la Uhindini pia ilielezwa kuwa chanzo kilikuwa moto kutoka katika moja ya vibanda vya chakula hali ambayo mpaka sasa Serikali inashindwa kukidhibiti.

No comments: