To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com                                                 To Advertise on this Blog please Call: +255 (0)656 56 13 14 or Email: maishablog@yahoo.com

Saturday, 17 September 2011

SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO...


Haya ni mabaki ya mabati na vyuma vilivyoteketea kwa moto
Moto bado unaendelea kuwaka taratibu huku watoto wakiokota mabaki ya bidhaa mbali mbali zilizoungua na moto
Vibaka wakitoka na vyuma chakavu katika banda la sido lililoungua kwa moto
Mabaki ya majiko ya mkaa na vigae vyake

Watu wengi wakitazama mabaki ya vitu sokoni hapo
soko limebaki ni uwanja tu hakuna kilichobakia

Jengo la sido mbeya nalo limeteketea kwa moto
HITILAFU YA UMEME NDIO KILIKUWA CHANZO CHA MOTO  
NA MWANDISHI WETU MAALUM KUTOKA ENEO LA TUKIO
ASUBUHI YA JANA  TAREHE 16.09.2011 NCHI IMEINGIA KATIKA JANGA LENGINE AMBAPO SOKO KUU JIPYA LA SIDO MWANJELWA MKOANI MBEYA LILITEKETEA KWA MOTO MAJIRA YA SAA 9:50AM ASUBUHI, MOTO HUO AMBAO ULISIMAMA UKIWAKA KWA MUDA WA MASAA MAWILI BILA KUZIMIKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA KUPOTEZA MALI ZA WATU WENGI. IKIWA NI MIAKA MICHACHE TUU  KUPITA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUPATA PIGO KUBWA BAADA YA SOKO KUU LA MWANJELWA KUUNGUA MOTO NA KUWALAZIMU WAANZE UPYA BIASHARA ZAO.

HABARI ZAIDI ZINASEMA BAADA YA MOTO HUO KUANZA ILICHUKUA MASAA MAWILI MPAKA MAGARI YA ZIMA MOTO KUFIKA NA KUANZA KAZI YA KUSAIDIA KUZIMA MOTO HUO AMBAPO WALIKUWA WAMECHELEWA HIVYO KUZIDI KUSABABISHA UPOTEVU WA MALI ZA WENYE MADUKA.

JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA JWTZ PAMOJA NA MIGAMBO WALIKUA KATIKA ENEO HILO  KUHAKIKISHA USALAMA KUTOKANA NA KUWA NA VIBAKA WENGI AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUIBA MALI ZA WANANCHI.

KATIKA TUKIO HILO LA MOTO KUCHOMA SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA BAADHI YA MAMBO YALITOKEA IKIWA NI PAMOJA NA MTU MMOJA KUGONGWA NA GARI ALIPO KUWA ANAJARIBU KWENDA KUOKOA MALI ZA WAFANYA BIASHARA HAO, PIA KULIKUWA KUNA MFANYA BIASHARA ALIKUA ANAZUIDA DUKA LAKE ILI WEZI WASIIBE KATIKA DUKA LAKE NA KUUNGUA KWA MOTO, INAHOFIWA HUYO NDIE MTU PEKEE AMEPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO HILO. PIA INARIPOTIWA KUWA KUNA MAMA MJAMZITO AMBAE ALIPATWA NA UCHUNGU NA KUTAKA KUJIFUNGUA KATIKA ENEO LA TUKIO LAKINI WASAMALIA WEMA WALIMWOKOA NA KUJIFUNGUA SALAMA.

WANANCHI WASIO NA MEMA AMBAO WAKATI JESHI LA POLISI LILIKUWA LIKIJARIBU KUWASAIDIA WATU, WANANCHI HAO WALIANZA KUPIGA MAWE MAGARI HAYO YA POLISI NA PIA KUWATUPIA MAWE MAPOLISI HATA HIVYO MAPOLISI HAO WALIFANIKIWA KUWASHINDA BAADA YA KUWATUPIA MABOMU YA MACHOZI.

AKIZUNGUMZA NA MMOJA WA WAFANYA BIASHARA JINA LAKE ANAITWA GODEN MWAKALINGA ALIELEZA KUWA CHANZO CHA MOTO HUO KILITOKANA NA HITILAFU YA UMEME KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA BWANA GHALIFA  NA KUSABABISHA MOTO HUO KUWAKA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA KATIKA SOKO HILO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA

No comments: